facebook likes

Saturday, July 6, 2013

HILI NDO GARI LA MBAO LILILO TENGENEZWA TANZANIA


Naibu waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Lazaro Nyalandu mwenye suti akipewa maelezo na afisa wa maliasili juu ya gari lililotengenezwa kwa miti ambalo linawavutia wengi bandani hapoNaibu waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Lazaro Nyalandu mwenye suti akipewa maelezo na afisa wa maliasili juu ya gari lililotengenezwa kwa miti ambalo linawavutia wengi bandani hapo Simba kivutio cha banda  (PICHA NA TULIZO KILAGA WA WIZARA YA MALIASILI NA UTALII)
…………………………………………………………….
Hussein Makame-MAELEZO
GARI ya mbao iliyobuniwa na mkazi wa kijiji cha Nyololo mkaoni Iringa, Keneth Mwangoka imeokoa shilingi Bilioni moja kwa mwaka kwa kuhamasisha kuhifadhi mazingira katika msitu wa Sao Hill ulioko mkoani humo.
Akizungumza na MAELEZO katika viwanja vya Maonesho ya 37 ya Sabasaba jijini Dar es Salaam jana, Afisa Misitu wa Wizara ya Maliasili na Utalii kutoka Msitu wa Sao Hill mkoani Iringa, Fidelis Mwanalikungu alisema gari hiyo ilibuniwa kwa kushirikiana na Kikundi cha Sanaa cha Imehe kilichopo katika kijiji cha Nyololo.
Alisema kikundi hicho kwa kutumia gari hiyo ambayo huvutia watu kuiangalia, kinaeleimisha vijini 58 vinavyozunguka msitu wa Sao Hill kudhibiti matumizi ya moto unawashwa na wakulima wakati wa kuandaa mashamba yao kwa ajili ya kilimo.
Alifafanua kuwa uhamasishaji huo umefanikiwa kupunguza moto kutoka matukio 143 yaliyokuwa yanasababisha hekta za misitu 500 hadi 1000 kwa mwaka hadi kufikia matukiio manne tu kwa mwaka yaliyounguza hekta 17 za misitu.

“Ukiweka hizo hekta 500 hadi 1,000 katika thamani ya fedha unakuta tulikuwa tunapoteza kuanzia Milioni 840 mpaka Bilioni moja kwa mwaka kutokana na kuungua kwa msitiu huo, sasa hii ni hasara kubwa” alisema Mwanalikungu.
Alisema kutokana na elimu inayotolewa kushirikisha kikundi hicho, wameweza kuhifadhi zingira ya msitu huo wa asili wa Serikali, vyanzo vya maji na kuhifadhi mazingira ya vijiji hivyo.
Aliongeza kuwa kwa mujibu wa utafiti uliofanyika mwaka 2009 uliobaini kuwa kutoka mwaka 2010 kurudi nyuma miaka 11 kulikuwa kuna matukio mengi ya moto yenye wastani wa matukio 143 kwa mwaka.
“Ilipofika mwaka 2011 tukaangalia ni mikakati gani tunaweza kuichukua kwa kuwashirikisha wanavijiji, ndipo tukagundua wazo la kusema tukiwa na gari kama hili linalovutia watu, tukaweka mabango ya kuelimisha tunaweza kufikisha ujumbe kwa urahisi zaidi” alisema Mwanalikungu.
Akizungumzia gari hiyo, Keneth Mwangoka gari hiyo aina ya Toyota Hiace aliinunua kutoka kwa mtu ambaye alitaka kuiuza kama chuma chakavu na aliitengeneza ili iweze kusaidia katika kuwavutia wanajiji na kupata njia ya kuwapata kwa urahisia wanakijiji a kufikisha ujumbe.
 Mwangoka ambaye ni fundi wa gari hiyo, alisema gari hiyo ina injini ya Toyota 1S, robu tatu ya vitu vilivyotengeneza ni mbao na inatumia mafuta lita moja kwa kilomita nane.

No comments:

COMMENTS

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...