Maud Chifamba ni
binti yatima aliyepoteza Wazazi wake wote wawili akiwa bado ana umri mdogo,ni
binti aliyekulia katika umaskini wa kutupwa nchini Zimbabwe,lakini pamoja na
mikasa yote hio aliyokutana nayo sasa ameweza kuweka rekodi mpya nchini
Zimbabwe kwa kuwa Mwanafunzi mwenye Umri mdogo zaidi kujiunga na Masomo ya Chuo
Kikuu nchini Zimbabwe ,haijawahi kutokea yeye ndio wa kwanza katika umri huo
kujiunga na Masomo ya Chuo Kikuu.Maud ambaye amezaliwa Novemba 19.1997 sasa
ameanza Masomo yake katika Chuo Kikuu cha zimbabwe akichukua Degree ya Uhasibu.
Chuuo Kikuu cha Zimbabwe ndio chuo kikongwe na kinachoheshimika nchini
Zimbabwe.
Maud natokea
katika familia ya Wawindaji kutoka katika Kijiji cha Chigetu katikati ya
Zimbabwe,Baba yake alifariki wakati akiwa na umri wa miaka mitano,Mama yake
amefariki mwaka uliopita,Kaka zake wawili
ni Wakulima walikuwa hawana uwezo wa kumsomesha hata katika Shule za
Selikali hii ilisababisha Maud mwenyewe kuanza kujisomea nyumbani,alijisomea
kwa juhudi kubwa na kwa uwezo wake wote,yeye mwenyewe Maud anasema “alisoma
kutwa nzima na wakati mwingine mpaka wakati wa usiku” Maud anasema kufa kwa
Wazazi wake kulimfanya atambue kwamba mafanikio yake yapo mikononi mwake.
Pia anaongeza kwa kusema ilibidi asome kwa bidii yeye mwenyewe kwa kuwa hakuna mtu wakunijali tena zaidi ya yeye mwenyewe.Kutokana na kubarikiwa na Mwenyezi Mungu uwezo mkubwa wa kuelewa ,hilo lilimfanya Walimu wamvushe Madarasa kutoka Darasa la tatu mpaka la sita.Akiwa na miaka nane alifanya mtihani wa Darasa la Saba na kupata alama za juu katika mitihani yake yote.kutokana ma taizo la kukosa pesa ilimfanya asijiunge na Masomo ya Sekondari,Maud akaamua kujisomea mwenyewenyumbani,na alijisomea mwenyewe kwa muda wa miaka miwili na kufanya mtihani badala ya kusoma miaka mine,baada ya hapo alijiunda na kidato cha tano na cha sita alisoma kwa mwaka mmoja na kupata alama zilizomwezesha kijiunga na masomo ya Chuo Kikuu.Mamlaka ya Mapato ya Zimbabwe (Zimbabwe Revenue Authority) ndio inayomfadhili Masomo yake ya Chuo Kikuu.

Haya mwanafunzi
wa Tanzania najua baada kusoma historia ya Maud utakuwa umejifunza kitu ,Hii
story inatufundisha haijalishi unatokea maisha magumu kiasi gani kama una nia
hakika utasonga mbele tu,siri kubwa ni kujituma,hata kama upo Shule ya Kata hio
sio sababu ya kukufanya wewe uiendelee na Masomo ya juu zaidi,nahakika kama
wewe ni Mwanafunzi mwenye nia ya kufanikiwa utakuwa umejifunza kitu kutokana na
historia ya MAUD
No comments:
Post a Comment