MFANYABIASHARA maarufu na Mmiliki
wa maduka ya Home Shopping Center (HSC), Said Mohamed Saad, ambaye wiki
iliyopita alimwagiwa tindikali maeneo ya Msasani City Mall, jijini Dar
es Salaam, sasa yuko Afrika Kusini kwa matibabu zaidi.
Wiki iliyopita majira ya saa moja
jioni, mfanyabiashara huyo alimwagiwa tindikali na mtu mmoja ambaye
hakufahamika na mara baada ya kutenda tukio hilo, mhusika alikimbia huku
mlinzi wa eneo hilo akijaribu kumkimbiza pasipo mafanikio baada ya
kuteleza na kuanguka.
Hatua hiyo ilitoa mwanya kwa mtuhumiwa kutoroka eneo la tukio kwa kutumia usafiri aina ya pikipiki.
Hapo awali ilidaiwa kuwa Saad alikuwa anaweza kuzungumza japo amefungwa mashine sehemu ya pua kwa ajili ya kumsaidia kupumua.
Matukio ya watu kumwagiwa tindikali yameonekana kushamiri nchini katika siku za hivi karibuni.
Tukio la kumwagiwa tindikali
mmiliki huyo wa Home Shopping Centre, limekuja ikiwa ni takribani wiki
mbili tangu Sheikh Mkuu wa Wilaya ya Arumeru, mkoani Arusha, Said Juma
Makamba naye ajeruhiwe vibaya usoni kwa kumwagiwa maji maji
yanayosadikiwa kuwa ni tindikali majira ya usiku akiwa nyumbani kwake.
No comments:
Post a Comment