HAUKUWA mwanzo mzuri wa maisha ya kocha
Manuel Pellegrini katika soka ya England, lakini leo amepata ushindi wa
kwanza Manchester City ikishinda 1-0 dhidi ya China Kusini, bao pekee la
Edin Dzeko dakika ya 21.
Vipigo viwili Afrika Kusini katika mechi
za mwanzo za Manchester City kujiandaa na msimu na kifo cha mama yake
mkubwa, Silvia, ambacho kilimrejesha ghafla nyumbani Chile ndani ya
mwezi mmoja tangu aanze kazi.
Ilitarajiwa Pellegrini angekaa Santiago
kwa zaidi, lakini amerejea kazini haraka katika ziara ya Kombe la
Barclays Asia na kutua Hong Kong saa 24 baada ya mazishi.
Kikosi cha Man City kilikuwa: Hart,
Zabaleta/Sinclair dk75, Kompany, Lescott, Clichy/Kolarov dk45, Milner,
Nasri, Barry/Rodwell dk55, Fernandinho/Javi Garcia dk65, Toure/Negredo
dk55 na Dzeko/Richards dk75.
China Kusini: Barry, Chak, Ticao, Cheng/Martins dk45, Naves, Lee Wai Lim/Lee Hong Lim dk52, Sealy, Tse, Joel, Kwok na Zhang.

Bao: Edin Dzeko akifunga bao la ushindi dakika ya 21 kwa kichwa akiunganisha krosi ya James Milner

Kwok Kin Pong wa China Kusini akipiga kichwa mpira dhiai ya James Milner

Amerudi kazini: Pellegrini amerejea kazini baada ya mazishi ya mama yake mkubwa


Kivutio: Negredo (kushoto) aling'ara leo akitokea benchi kama anavyoonekana akimtoka Kolarov (kulia)

Mikono salama: Hart aliokoa vizuri leo

Mlinzi: Kompany akimkimbiza mshambuliaji wa China Kusini

Nyomi ya mashabiki
No comments:
Post a Comment