KLABU ya Arsenal imeiambia Roma iongeze
dau lake ililotoa kwa ajili ya mshambuliaji Gervinho. Roma imetoa ofa ya
Pauni Milioni 6.8 na Arsenal inataka Pauni Milioni 8.6.
Mshambuliaji wa Roma, Pablo Osvaldo pia amekuwa katika mjadala. Fulham pia wanamtaka Osvaldo.
Msaka vipaji wa Arsenal, Everton
Gushiken alimuangalia kiungo wa Atletico Mineiro, Bernard dhidi ya
Olimpia usiku wa jana katika Fainali ya Copa Libertadores.

Yuko njiani: Roma inamtaka Gervinho ahamie Italia kutoka Arsenal

Dili la kubadilishana: Pablo Osvaldo (kushoto) anaweza kuhusishwa kwenye dili la uhamisho wa Gervinho
No comments:
Post a Comment