COASTAL
Union ya Tanga imeonyesha iko sawa kuelekea msimu ujao wa Ligi Kuu ya
Vodacom Tanzania Bara baada ya jioni hii kuilaza 1-0 URA ya Uganda
kwenye Uwanja wa Mkwakwani, Tanga.
Shujaa
wa Coastal jioni ya leo alikuwa ni mshambuliaji mpya, Keneth Masumbuko
aliyesajiliwa kutoka Polisi Morogoro, ambaye alifunga bao hilo pekee la
ushindi.
Masumbuko alifunga bao hilo dakika ya 70, akiunganisha pasi ya Uhuru Suleiman aliyewatoka mabeki wa URA.
Kwa
ushindi huo, Coastal inayofundishwa na kocha Mzanzibari, Hemed Morocco
imefanya kile ambacho vigogo wa soka nchini, Simba na Yanga walishindwa
mbele ya Watoza Kodi hao wa Uganda.
URA iliifunga Simba SC 2-1 kabla ya kulazimishwa sare ya 2-2 na Yanga Uwanja wa Dar es Salaam wikiendi iliyopita.
Mchezo
huo ulikuwa na kasi ya vuta ni kuvute ambapo mpaka kipindi cha kwanza
kinamalizika hakuna timu iliyokuwa imeona lango la mwenzake, kipindi cha
pili timu zote ziliingia uwanja hapo zikiwa na hari na nguvu ya kutaka
kuibuka na ushindi.
Kipindi
cha pili Coastal Union walifanya mabadiliko yaliyoweza kuzaa matunda
kwa kuwatoa Daniel Lyanga ambaye nafasi yake ilichukuliwa Selamani
Kassim Selembe kwenye dakika ya 54 kuingia kwa mchezaji huyo kuliongeza
nguvu ya mashambulizi na kuweza kufanikiwa kucheza nusu uwanja.
Wachezaji
wengine walioingia kipindi cha pili na kuongeza kasi ya mashambulizi
yaliyofanikiwa kudhaa matunda ni Abdi Banda aliyechukua nafasi ya
Othumani Tamim dakika 55 huku dakika moja baadae akatoka Hamadi Juma na
kuingia Mbwana Kibacha mabadiliko hayoa yaliweza kuleta mafanikio
makubwa hasa kwenye kikosi hicho ambacho kinajiandaa na Ligi kuu
Tanzania bara.
Wakionekana
kucheza kwa kujipanga na kujituma, Coastal Union waliweza kufanya
mashambulio ya mara kwa mara langoni mwa URA huku wachezaji wake
wakipiga mashuti yaliyokuwa yakiupanguliwa na mlinda mlando wa URA Bwete
Brian.
Kutokana
na mashambulio hayo Coastal Union waliweza nao kujipanga na kuweza
kuthibiti vizuri safu yao ya ulinzi kwa kuwa makini na wachezaji wa URA
hali ambayo iliwapa wakati mgumu kufika langoni mwa Coastal Union ambapo
katika dakika ya 83 Coastal Union walifanya mabadiliko ya kumtoa Keneth
Masumbuko na kumuingiza Pius Kisambale.
Huku
URA walifanya mabadiko kwenye dakika ya 84 wakimtoaWalulya Derrick na
kumuingiza Lugya Ronald ambapo licha ya kucheza vema lakini walishindwa
kubadilisha matokeo kwenye mechi hiyo ambayo ilikuwa na upinzani mkubwa
kwa timu zote mbili.
Wachezaji
walioweza kuwakonga nyoyo vilivyo mashabiki wa Coastal Union ya Tanga
ni Uhuru Selemani ambaye alikuwa mwiba kwa wachezaji wa Uganda huku
mashabiki wa soka waliojitokeza kwenye mechi hiyo, wakimshangilia
vilivyo kila alipokuwa akigusa mpira,huku wachezaji wengine akiwemo Juma
Nyoso,Haruna Moshi "Boban"wakiwafurahisha mashabiki kwa kucheza soka
nzuri .
Kikosi
cha Coastal Union leo kiliwakilishwa na mlinda mlango Shaban Kado,Hamad
Juma,Othuman Tamim,Markus Ndehele,Juma Said "Nyoso"Jerry Santos,Uhuru
Seleman,Crispian Odula,Daniel Lyanga,Haruna Moshi Boban na Keneth
Masumbuko.
Kwa
upande wa URA waliwakilishwa na Bwete Brian, Walulya Derrick, Sekijo
Samweli, Munaaba Allan, Docca Musa, Agaba Oscar, Nkugwe Elkamack, Feri
Ally, Ngama Emanuel, Lutimba Yayo, Kasibante James, Mugabi Yasin, Ganya
Willy na Lugya Ronald.
Ameng'ara leo; Suleiman Kassim 'Selembe' ameng'ara leo Coastal ikiichapa URA 1-0 |
source:binzubeiry
No comments:
Post a Comment