facebook likes

Thursday, July 25, 2013

OFFICIAL: YANGA YAMALIZANA RASMI NA HAMIS KIIZA


Sakata la usajili la mshambuliaji Uganda anayekipiga kwa mabingwa wa ligi kuu ya Tanzania Dar Young African Hamisi Kiiza limefikia tamati rasmi baada ya Yanga na Kiiza kukubaliana kimsingi kuongeza mkataba mpya wa mshambuliaji huyo.

Kwa mujibu wa Hamis Kiiza  anatarajia kusaini mkataba wa miaka miwili kabla hajaondoka kwenda kwao Uganda.
"Tumefikiana na klabu yangu - sasa nitaongeza mkataba na kuendelea kuitumikia klabu ya Yanga msimu ujao. Baada ya kumaliza taratibu zote za kusaini mkataba mpya nitarudi nyumbani Uganda mara moja kabla ya kurudi kuja kujiunga rasmi na wenzangu kwenye pre-season," Kiiza alisema. 

No comments:

COMMENTS

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...