KWA MARA YA KWANZA NDANI YA MIAKA 5 BARCELONA WAZIDIWA NGUVU YA KILA KITU NA PEP GUARDIOLA'S BAYERN MUNICH.
KOCHA wa Bayern Munich, Pep Guardiola
ameifunga timu yake ya zamani, Barcelona mabao 2-0 katika mchezo wa
kirafiki mjini Munich leo.
Philipp Lahm alifunga bao la kwanza
dakika ya 14 na timu zikaenda kupumzika matokeo ya 1-0, kabla ya Bayern
kupata bao la pili dakika ya 87 lililofungwa Mario Mandzukic.
Kikosi cha Bayern Munich
kilikuwa: Neuer/Starke dk46, Rafinha, Dante/Van Buyten dk59, Boateng,
Alaba, Thiago, Lahm/Gustavo dk59, Kroos, Ribery, Robben/Shaqiri dk46 na
Muller/Mandzukic dk46.
Barcelona: Pinto/Oier
dk46, Montoya/Kiko dk46, Bartra/Gomez dk46, Mascherano/Planas dk46,
Adriano/Patric dk46, Song/Espinosa dk46, Sergi Roberto/Ilie dk46, Dos
Santos/Quintilla dk46, Tello/Joan Roman dk46, Messi/Dongou dk46 na
Alexis/Dani Nieto dk46.
Amefunga: Philip Lahm (katikati) alifunga bao la kwanza la Bayern Munich
Mwendo mzuri: Pep Guardiola ameifunga timu yake ya zamani, Barcelona
Kilio: Nahodha wa Barcelona, Messi alicheza ovyo kipindi cha kwanza akatolewa
La pili: Mario Mandzukic akifunga la pili
Hakuna njia: Thiago (kushoto) na Boateng (kulia) wakimdhibiti Messi
Frank Ribery akipambana na Marc Bartra
Guardiola anaonekana kuwa na kikosi kizuri
No comments:
Post a Comment