facebook likes

Friday, July 26, 2013

Stori kamili kuhusu Lebron James kutoichezea tena timu ya taifa ya Marekani.


lebron
Star wa NBA Lebron James huenda asiichezee tena timu ya taifa ya Marekani kwenye michuano mbalimbali ya kimataifa ambapo taarifa iliyotoka kwa walio karibu nae  mkali huyu wa Miami Heat ambayo mwezi uliopita aliiongoza kutwaa ubingwa wake wa tatu wa NBA, ni kwamba amechoshwa na kucheza mechi nyingi za timu yake ya NBA na timu ya taifa hivyo wakati timu ya taifa ikicheza, yeye atakuwa karibu zaidi na familia yake.
L23 kama lilivyo jina lake, ana familia changa ambayo anahitaji kuwa karibu nayo na anahisi kuwa hakuna ulazima wa yeye kuwepo kuisaidia timu ya taifa kwani kuna wachezaji wengine wanaoweza kujaza nafasi yake.
Lebron James ameamua kuwatosa wenzie Team USA.
Lebron James ameamua kuwatosa wenzie Team USA.
Wakati Lebron akiwaza kuikacha Drea Team, Nyota wa Oklahoma City Thunder Kevin Durant ametangaza nia ya kuichezea timu ya taifa ya Marekani kwenye mashindano ya dunia mwakani na ameungwa mkono na staa mwingine wa Minesotta Timberwolves Kevin Love ambaye ametangaza kuendelea kuwa sehemu ya timu ya taifa hasa kwenye michuano ya mwakani ya dunia kwa timu za taifa za Kikapu ambapo Marekani ndio mabingwa watetezi.

No comments:

COMMENTS

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...