KLABU ya Chelsea imekamilisha ziara yake
ya Asia kwa ushindi wa kishindo wa mabao 8-1 dhidi ya Indonesia All
Stars na kocha Jose Mourinho anarejea nyumbani nafsi yake ikiwa
imerishika na wachezaji waliowasili mapema.
Romelu Lukaku ameonyesha uwezo wa
kufunga kwa kufunga mabao manne katika dakika 135 na Bertrand Traore pia
ameonyesha ni kiungo hodari.
Kevin De Bruyne amevutia mjini Bangkok na Kuala Lumpur na mjini Jakarta, Nathaniel Chalobah alikuwa miongoni mwa waliovutia.
Mabao ya Chelsea yalifungwa na Hazard
kwa penalti dakika ya 21, Ramires dakika ya 29 na 56, Ba dakika ya 32,
Terry dakika ya 45, Traore dakika ya 50 na Lukaku dakika ya 52 na 65.
Bao la kufutia machozi la Indonesia All-Stars limefungwa na Kalas aliyejifunga dakika ya 67.
Kikosi cha Chelsea
kilikuwa: Blackman/Schwarzer dk46, Wallace/Ivanovic dk46, Cahill,
Terry/Kalas dk46, Bertrand/Cole dk46, Chalobah/Essien dk46, Van
Ginkel/McEachran dk60, Ramires/Feruz dk60, Hazard/Piazon dk60,
Moses/Traore dk46 na Ba/Lukaku dk46.
Wakali wa mabao: Kutoka kushoto Wallace, Demba Ba na Ramires (wakishangilia ushindi wa Chelsea leo
Nahodha John Terry akishangilia na Gary Cahill
Mashabiki Indonesia wakiishangilia Chelsea
Jose Mourinho akilalama
Nahodha wa Chelsea, John Terry (kulia) akishangilia na wachezaji wenzake baada ya kufunga
Eden Hazard akifunga kwa penalti
Ramires akifunga
Demba Ba (kushoto) na Ramires wakishangilia
No comments:
Post a Comment