RIPOTI ya wiki hii imegundua kuwa watu wengi hasa wale wenye tabia ya kuondoa nta ya sikio huwa katika hatari ya kuwa viziwi maishani mwao.
Katika uchunguzi
wake, Ripoti ya Wiki ilifanya mahojiano na mtaalamu wa magonjwa
mbalimbali ya binadamu, Dr. Bujiku Kayegeji na kung’amua kuwa watu wengi
huona nta iliyopo sikioni kama uchafu hivyo hujijengea tabia ya
kuiondoa mara kwa mara bila kujua kuwa huwa na kazi muhimu ndani ya
sikio.
Mtaalamu huyo alisema kuwa, nta ina kazi nyingi. Kazi hizo ni kama vile kuzuia vijidudu vya magonjwa visiathiri sehemu ya ndani ya sikio, kuzuia vumbi, kulainisha ngozi ya ndani ya sikio na kuhusika katika kuchuja sauti sambamba na viungo vingine vilivyopo ndani ya sikio.
Kutokana na faida hizo, endapo mtu atakuwa na tabia ya kuiondoa nta kila mara, tena kwa kutumia vijiti vya pamba ‘pamba stick,’ huwa katika hatari ya kukosa faida zilizoainishwa hapo awali na kujisababishia madhara kama vile muwasho ndani ya sikio (itching) kutokana na bakteria wa fangasi na vumbi ambalo litakuwa likiingia bila kizuizi.
Hatari
ya pili ni kukauka kwa ngozi ya ndani ya sikio na maumivu makali hasa
kama mtu huyo atakuwa katika mazingira yenye kelele nyingi na mwisho
kabisa ni kuharibika kwa ngoma ya sikio na mfumo mzima wa usikivu.
Hata hivyo, pamoja na faida hizo za nta ndani ya sikio ni vyema mtu akajua kwamba nta ikizidi sikioni huweza kusababisha
kuziba kwa sikio, kusababisha kizunguzungu na kuhisi karaha
(discomfort) hivyo ni vyema kama mtu atakuwa akiondoa nta hiyo angalau
mara moja kwa kila miezi miwili kwa afya yake.
“Nta huwa uchafu kama itazidi sikioni ni vyema kujiwekea ratiba ya kuondoa kila baada ya miezi miwili kuliko kufanya hivyo kila mara,” alisema Dr. Bujiku.
Credit: GPL

Mtaalamu huyo alisema kuwa, nta ina kazi nyingi. Kazi hizo ni kama vile kuzuia vijidudu vya magonjwa visiathiri sehemu ya ndani ya sikio, kuzuia vumbi, kulainisha ngozi ya ndani ya sikio na kuhusika katika kuchuja sauti sambamba na viungo vingine vilivyopo ndani ya sikio.
Kutokana na faida hizo, endapo mtu atakuwa na tabia ya kuiondoa nta kila mara, tena kwa kutumia vijiti vya pamba ‘pamba stick,’ huwa katika hatari ya kukosa faida zilizoainishwa hapo awali na kujisababishia madhara kama vile muwasho ndani ya sikio (itching) kutokana na bakteria wa fangasi na vumbi ambalo litakuwa likiingia bila kizuizi.

“Nta huwa uchafu kama itazidi sikioni ni vyema kujiwekea ratiba ya kuondoa kila baada ya miezi miwili kuliko kufanya hivyo kila mara,” alisema Dr. Bujiku.
Credit: GPL
No comments:
Post a Comment