"Mke wa ndoa inadaiwa ilipanga na majambazi wamuue mumewe ili aweze kumiliki utajiri alionao"
Arusha. Mfanyabiashara wa madini ya Tanzanite mkazi wa Moshono, anadaiwa kutaka kuuawawa na mke wake wa ndoa ili aridhi mali.
Mwanamke huyo alikamatwa na polisi Julai 19 mwaka huu baada ya mpango
wake wa kumuua mumewe wa ndoa kwa kutumia majambazi anaodaiwa kuwalipa
Sh30 milioni kama malipo ya awali.
Inadaiwa licha ya kutaka kumuua mumewe waliyezaa naye watoto wawili,
alipanga kumuua mtoto wa kwanza wa kiume wa mume wake aliyezaa na
mwanamke mwingine. Mtoto huyo anaishi mkoani Kagera.
"sikuamini kama itafika siku mke wangu wa ndoa, tena ya Kikristo
atafikiria kunitoa roho kwa sababu ya mali, wakati nimempa yeye na
familia yake kila wanachohitaji duniani" alisema mwanaume huyo huku
akitokwa na machozi.
Alidai kuwa tukio hilo limempa mafundisho tofauti na alivyokuwa anafikiri awali.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Liberatus Sabas, alipotakiwa
kuzungumzia suala hilo hakukiri wala kukanusha kukamatwa kwa wahusika
wanne wa mpango huo, lakini alisema atatoa taarifa rasmi baada ya
mahojiano na watuhumiwa.
Taarifa za mpango huo zinadai kuwa mwanamke huyo ktk kutimiza azma yake,
alimfuata dereva teksi mmoja eneo la Kijenge kumtafutia watu wanaoweza
kufanya mauaji hayo.
Inadaiwa dereva huyo aliwasiliana na 'wahusika' na kuwapa mpango huo,
lakini mmoja wao hakutaka kushiriki' aliamua kufikisha suala hilo Polisi
walioweka mtego na kuwanasa.
Mhusika huyo ambaye hakutaka kutajwa alithibitisha kushirikishwa na
kulipwa Sh5 milioni, ikiwa ni malipo ya awali kati ya Sh20 milioni
alizoahidiwa.
Hata hivyo, baada ya kukwama mpango wa awali mwanamke huyo aliamua
kutimiza azma yake kwa kumtumia dereva teksi huyo huyo kumtafutia wauaji
wengine.
Inaelezwa dereva teksi huyo alifanikisha kukodisha wauaji wengine na
kuwasafirisha hadi mkoani Kagera kwa ajili ya kufanya mauaji ya mtoto wa
kwanza wa kiume wa mume wake aliyezaa na mwanamke mwingine.
Baada ya kupata taarifa hizo, Polisi waliweka mtego na kufanikiwa
kuwanasa wahusika wawili mkoani Kagera, hivi sasa wanahojiwa Kituo Kikuu
Cha Polisi Arusha.
Polisi baada ya kuwanasa watuhumiwa hao, walianza upelelezi na
kufanikiwa kukamata mwingine na mwanamke huyo ambao hadi sasa
wanaendelea kuhojiwa.
Inadaiwa baada ya wahusika kunaswa mwanamke huyo alijaribu kutoa Sh50
milioni, ili kuzima sakata hilo, lakini jitihada hizo ziliishia kwenye
mtego wa Polisi waliojipanga na kumnasa.
Taarifa za kunaswa kwa mwanamke huyo zilianza kusambaa mwishoni mwa wiki iliyopita, kabla ya kuthibitishwa na mumewe na Polisi.
No comments:
Post a Comment