facebook likes

Thursday, July 25, 2013

Kaka wa Michael Jackson ameiona video ya P Square ‘Personally’ na kuyazungumza haya


.
.
Wakati mwingine nikitazama kwa jicho jingine naona ni jinsi gani P Square pamoja na mapenzi waliyonayo kwa Michael Jackson, ni jinsigani wanavyojua kujipanga kwa ajili ya promo ya wao wenyewe kuzidi kujitangaza..
Ni mwezi mmoja tu umepita tangu watoe video ya single yao mpya ya ‘Personally’ ambayo ndani yake wamemuenzi mwimbaji staa Michael Jackson kwa kucheza kama alivyokua akifanya wakati wa uhai wake, lakini ndani ya hiki kipindi kifupi toka video itoke… wakali hawa wa Nigeria wamefanya juu chini mpaka video hii ikaifikia familia ya MJ.
Jermain Jackson ambae ni kaka wa Michael Jackson amezungumza, kawasifia na kuwashukuru P Square kwanza kwa uamuzi wao wa kumuenzi MJ, ni kitu kilichomfurahisha sana kuanzia kwenye uimbaji na uchezaji ndani ya video yenyewe, kamalizia kwa kusema P Square ‘all the best, thank you’

No comments:

COMMENTS

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...