KOCHA Brendan Rodgers anaamini mapokezi mazuri aliyoyapata Luis Suarez akirejea kazini leo yanaweza kumfanya abaki Liverpool.
Mshambuliaji huyo wa Uruguay, ambaye
anatakiwa sana na Arsenal, alipata mapokezi mazuri mbele ya umati wa
watu 95,446 wakati alipoingia uwanjani akitokea benchi dakika ya 72 na
kuiwezesha Liverpool kushinda 2-0 dhidi ya Melbourne Victory Uwanja wa
MCG.

Peke yake: Suarez akitembea chini ya jukwaa leo baada ya Liverpool kuilaza 2-0 Melbourne

Amerudi kazini: Suarez amecheza mechi ya kwanza leo Liverpool tangu Aprili 21

Mkeka: Suarez alianzia benchi kabla ya kuingia dakika ya 70
Suarez alitengeneza bao la pili la
Liverpool akimpelekea krosi Iago Aspas. Steven Gerrard alifunga bao la
kwanza akifanya kazi na kumalizia yeye mwenyewe.
Arsenal imeipa Liverpool jana ofa ya
Pauni 40,000,001 kujaribu kumsajili Suarez, lakini Rodgers ameendeela
kusistiza juu ya kutotaka kumuuza mchezaji huyo.

Suarez akionyesha ufundi

Suarez alianza pole pole mchezo wa leo, lakini akachanganya dakika tano za mwisho

Suarez bado anapendwa na mashabiki wa Liverpool

Suarez akisaini autograph katika Uwanja wa Kriketi wa Melbourne

Dole: Suarez akiwapa salamu ya aina yake mashabiki wa Liverpool

Anamtoka mtu
No comments:
Post a Comment