- Anaeleza pindi anapokuwa mjamzito hapati vyakula vinavyohitajika kama lishe hivyo analazimika kutumia muda mwingi kufanya vibarua vya kumwingizia kipato, hivyo kutokana na uhaba wa fedha hulazimika kwa siku kupata mlo mmoja.
Wanaume wengine hukimbia wenza baada ya kuwapa mimba
Arumeru. Hali ngumu ya maisha ni
chanzo cha lishe duni kwa mama mjamzito hata mtoto anayetarajiwa
kuzaliwa kwa kuwa wengi wao hutumia muda mwingi kujitafutia kipato.
Imekuwa ni jambo la kawaida kwa jamii ya Kimasai
hasa wanaume kuwaacha wanawake zao nyumbani huku wakiwaachia majukumu
yote wanawake hao wakihangaika kutafuta maisha ili waweze kuendesha
maisha inayomzunguuka.
Mama mjamzito anatakiwa ale chakula kwa siku mara
nne asubuhi apate kifungua kinywa na kuanzia saa 3 hadi saa 4 asubuhi
anatakiwa apike uji ambao ni lishe wenye mchanganyiko kama mahindi,
mtama mweupe na karanga ambao akinywa utamjenga mtoto aliye tumboni.
Vyakula hivyo vitamsaidia kutengeneza virutubisho muhimu katika maziwa ambayo anatarajiwa kunyonya mtoto atakayezaliwa.
Hivyo, mtoto anapozaliwa zaidi ya saa moja
anyonye maziwa ya mama yake kwanza ambayo yana virutubisho vyote vya
kumlinda mtoto huyo.
Hata hivyo, hali ni tofauti kwa jamii hiyo ya
Kimasai ambako asilimia kubwa ya wanaume wakishawapa mimba wake zao,
wengi husafiri na kwenda nje ya mkoa wao kutafuta maisha au hata kuoa
mke mwingine .
Neema Sanare, mkazi wa eneo la Losikito Kata ya
Mwandeti Wilaya ya Arumeru Magharibi mkoani Arusha anaeleza kuwa yeye ni
mjamzito kwa sasa ana mtoto mwenye umri wa miaka mitatu lakini pindi
anapokuwa mjamzito hadi kujifungua mume wake huwa anaondoka kwenda kwa
mke mwingine.
Anaeleza pindi anapokuwa mjamzito hapati vyakula
vinavyohitajika kama lishe hivyo analazimika kutumia muda mwingi kufanya
vibarua vya kumwingizia kipato, hivyo kutokana na uhaba wa fedha
hulazimika kwa siku kupata mlo mmoja.
Sanare anasimulia akiwa na hali hiyo au analea
mtoto, mume wake huwa hamjali na anahamia kwa mwanamke mwingine au
anasafiri kwenda Kenya kutafuta maisha.
“Kama hivi nina wakati mgumu ni kawaida yake
nikishakuwa mjamzito hadi najifungua, mwanaume haonekani hadi mtoto
atakapofikia umri wa miaka mitatu.
Anasema alipojifungua mtoto wake wa kwanza mume
wake aliondoka na kumwacha akiwa na mama mkwe ambaye alikuwa
anamtunza, lakini mtoto alipofika miezi minne alilazimika kufanya
shughuli ya kumpatia kipato ili aweze kuishi.
No comments:
Post a Comment