facebook likes

Saturday, August 3, 2013

MAONI YA RASIMU YA KATIBA KWA WATANZANIA WOTE WANAOISHI MAREKANI


Tunapenda kutumia fursa hii kuwajulisha juu ya kamati maalum ya muda – Kamati ya Mapendekezo ya Katiba ya Tanzania (KAMKATA). 
Lengo la kamati hii ni kuhakikisha kwamba kila Mtanzania aishie Marekani anapata fursa ya kushiriki kikamilifu katika jambo la kihistoria la kutoa maoni na mapendekezo kuhusu Rasimu ya Katiba iliotolewa na Tume ya Marekebisho ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mnamo June 3, 2013.
Kamati hii imeundwa kwa ushirikiano wa baadhi ya wanajumuia na viongozi kadhaa wa jamii za Watanzania waishio hapa nchini. 
KAMKATA ni chombo cha kujitolea, kinachofanya kazi zake kwa kufuata utaratibu uliotolewa na Mwenyekiti wa Tume ya Marekebisho ya Katiba – Mheshimiwa Jaji Mstaafu Joseph Warioba. Unaweza kutembelea tovuti ya Tume Taifa ya Marekebisho ya Katiba taifa kwa kujionea shughuli mbali mbali na hatua mbalimbali zilikokwishafanywa na zinazoendelea kufanywa na Tume hii ya Taifa. Vilevile kwenye tovuti hiyo unaweza kupata Rasimu ya kwanza ya Katiba mpya ambayo ndio inatolewa maoni sasa hivi www.katiba.go.tz
  
KAMKATA inatarajia kuendendesh shughuli zake kwa kushirikiana na ofisi ya ubalozi wa Tanzania hapa Marekani na makundi mbalimbali ya Jumuia za Watanzania hapa nchini.

Viongozi wa kamati hii ni:

Nassor Ally – Katibu
Anthony Tinru - Mjumbe
Kadari Lincoln Singo – Mjumbe
Erick Byorwango  – Mjumbe
Rabia Dahal – Mjumbe

Njia tutakazozitumia katika kuwasiliana na wanajamii ni pamoja na kupitia kwenye Jumuia za Watanzania, vyombo vya matangazo, tovuti ya kamati, (iko kwenye matengenezo ya mwisho) barua pepe katibatz@yahoo.com , na kwa njia za simu (415)316-5247

Kikomo cha zoezi hili ni August 25, 2013.

Utakapopata taarifa hizi, unaweza kuanza mawasiliano na kamati hii na kuleta maoni yako kwa kutumia njia ya mawasiliano iliyopo hapo juu.  Vilevile tunashauri kuwafahamisha wengine na kupeleka ujumbe huu kwenye uongozi au jamii yako.

Tunategemea kila mmoja wetu atakua pamoja na kamati hii na kutoa ushiriki mpana kwa kuchangia na kutoa mawazo yake kwa uhuru na uwazi.

Uwezekano wa zoezi hili utatokana na ushirikiano wetu sote.

Tunashukuru sana.
KAMATI YA RASIMU YA KATIBA (KAMKATA) MAREKANI.

No comments:

COMMENTS

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...