facebook likes

Saturday, August 3, 2013

Mbunge amwaga machozi mbele ya Waziri Maghembe


Moto
Nyumba ya Mbunge wa Masasi Mjini, Mariam Kasembe (CCM),iliyoteketezwa kwa moto na wananchi katika vurugu zilizotokea Machi, mwaka huu.
 
Mbunge wa Masasi Mjini, Mariam Kasembe (CCM), amemwaga machozi mbele ya Waziri wa Maji, Profesa Jumanne Maghembe, baada ya kutembele nyumba yake iliyoteketezwa kwa moto na wananchi katika vurugu zilizotokea Machi, mwaka huu.
Tukio hilo lilitokea juzi wakati Waziri Profesa Maghembe kutembelea maeneo mbalimbali ya serikali yaliyoharibiwa na wananchi katika vurugu hizo na kujionea uharibifu mkubwa.
Baada ua Waziri Maghembe kufika mahali ilipokuwapo nyumba ya mbunge huyo, alishuhudia pia uharibifu mkubwa uliofanywa na wananchi hao.
“Kutokana na hali hii, mpaka sasa familia yangu haina mahali pa kuishi. Tumeendelea kuishi kwenye kontena kwa zaidi ya miezi sita sasa,” Mbunge Kasembe alimweleza Waziri Maghembe huku akibubujikwa machozi.
“Hali ni mbaya sana, uharibifu ni mkubwa, lakini tusonge mbele na tusikubali uharibifu kama huu kutokea tena,” alisema Profesa Maghembe.
Aidha, Waziri Maghembe aliuagiza uongozi wa Halmashauri ya Masasi kuangalia namna ya kumsaidia mbunge huyo.

No comments:

COMMENTS

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...