Mkuu
wa ujumbe wa uangalizi kutoka Muungano wa Afrika nchini Zimbabwe,
Olusegun Obasanjo amesema uchaguzi mkuu wa hapo Jumatano ulikua huru na
haki. Matokeo ya awali yanaoyesha Rais Robert Mugabe na chama tawala cha
Zanu PF wakiongoza kwa kura nyingi
Chama
hicho tayari kimedai ushindi. Msemaji wa chama hicho Rugare Gumbo
alisema chama hicho kilitarajiwa kushinda kiasi ya asilimia 70 ya kura
hizo
Lakini
mpinzani wa Mugabe, Morgan Tsvangirai, amesema uchaguzi huo ni wa uongo
na kusema udanganyifu uliofanyika una maana uchaguzi huo haukubaliki.
Waangalizi
kutoka Umoja wa Afrika na jumuia ya maendeleo kusini mwa Afrika
wanatarajiwa kutoa tamko rasmi hii leo kuhusu uchaguzi huo.
Bw.
Obasanjo amesema kulikua na visa kadhaa wakati wa shughuli ya kupiga
kura. Hata hivyo amesema visa hivyo haviwezi kutajwa kuwa na uzito wa
kubatilisha au kufuta matokeo ya kura.
Msimamo wa Muungano wa Afrika unatofautiana na ule wa kundi la uangalizi la Zimbabwe Election Support Network.
Kundi
hilo ambalo ndilo kubwa zaidi linalochunguza kura ya Zimbabwe
limekashifu uchaguzi mkuu na kusema ulikuwa na dosari nyingi. Hii ni kwa
sababu watu milioni moja walizuiwa kupiga kura.
Huku
upande wa Rais Mugabe ulitangaza kushinda uchaguzi na Morgan Tsvangirai
akipinga ni dhahiri kwamba Zimbabwe ingali na mgawanyiko mkubwa wa
kisiasa.
No comments:
Post a Comment