Wanaume wawili wameshikiliwa na polisi kwa tuhuma za kutishia kumbaka mwanaharakati Cariline Criado-Perez kupitia ukurasa wa twitter.
yote hayo yalianza kutokana na kampeni ya kutaka kuwekwa picha ya mwanamke kwenye noti ya pound 10 ya uingereza iliyokuwa ikifanywa na Perez.
Masaa machache baada ya picha hiyo kupigwa, mwanaharakati huyo alishambuliwa kwa tweets za matusi na vitisho vya kumbaka na kumuua nyumbani kwake vilivyosambaa huku zikiambatana na adress ya mahali anapoishi.
"vitisho vikubwa sana, huku wakielezea kwa udani kitakachinitokea, na kulikua na vitisho vya kubaka na kuua." amesema Perez.
Huku akielezea kuwa alikuwa akipokea takribani tweet moja ndani ya dakika moja, Perez aliendelea kupokea tweets za kumshambulia kwa siku kadhaa kutoka kwa watu wasiojuikana (anonymos) ambao alikuwa akiwa block badala yake wanafungua akaunti mpya.
Wengine walimshauri kuwapuuzia lakini hakufanya hivyo na aliripoti polisi, na mpaka sasa wanaume wawili wameshikiliwa na wengine wengi wanaweza kufatia.
"Nadhani watu wengi waliokuwa wakinitumia tweets walidhani hakuna chochote kinachoweza kuwatokea, wengine walinicheka niliposema nita dili na wao, kwasababu walidhani hakuna kitachofanyika, na watu wote walio twetter inabidi wasimame na kusema hapana, kuna sheria na hivyo tutadili na nao". aliemdelea kusema
Zaidi ya watu 120,000 wamesaini ombi la kuitaka tweeter ku-install kitufe cha kuripoti unyanyasaji kwa kila tweet na kwa kila platform, na kuajiri wafanyakazi zaidi kwa ajili ya kuangalia pamoja na kuziondoa tweets za vitisho na manyanyaso. Tweeter wametegemea kuboresha mfumo mpya hivi karibuni kwaajili ya kuripoti matusi.
Perez amesema mpaka jana amepokea tweets 2 kitu ambacho kinaonyesha kupunguwa kwa tweets hizo, na ushauri wake ni watu kuripoti polisi, kwani vitisho vya kuuwawa ni makosa hata kama ni kupitia mtandao wa tweeter.
Tanzania tumeshuhudia tweets na post za facebook nyingi zikiwanyanyasa na kuwatukana matusi watu, lakini kwasababu hatuna sheria za mitandao (Cyber Laws) watu wanapeta tu.
No comments:
Post a Comment