“Kilimo ni ajira kwa
vijana, kama wataandamana kwa kudai kilimo niko tayari kuwapokea kuliko kama
wataandamana kwa kudai ajira na mambo mengine, nataka vijana wapewe fedha na
ardhi ili wajikombe kwa shughuli zao,” Christopher Chiza
Dodoma. Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika, Christopher
Chiza, jana alihamasisha vijana kufanya maandamano makubwa kwenda kwenye wizara
yake kudai mabilioni ya fedha maarufu za JK ilimradi kama wataahidi kutumia
fedha hizo kwa ajili ya kilimo, atakuwa tayari kuyapokea.
Kauli mbinu ya maonyesho
ya mwaka huu ni zalisha Mazao ya Kilimo na Mifugo kuleta Mahitaji ya Soko.
Waziri huyo alisema,
maandamano ya vijana hata kama yatakuwa kwa maelfu lakini yakilenga kupata
fedha kwa shughuli za kilimo, hayatakuwa na madhara na atayapokea.
“Kilimo ni ajira kwa vijana, kama wataandamana kwa kudai kilimo
niko tayari kuwapokea kuliko kama wataandamana kwa kudai ajira na mambo
mengine, nataka vijana wapewe fedha na ardhi ili wajikombe kwa shughuli zao,”
alisema Chiza.
Kutokana na kauli hiyo, aliwaita wakuu wa wilaya za mikoa ya
Dodoma na Singida ambao waliapishwa mbele yake ili kujua kama wanamipango
madhubuti katika wilaya zao kwa ajili ya kuwapa ardhi vijana.
Wakuu wa wilaya zote waliahidi mbele yake kuwa wataendeleza
utaratibu wa kutenga ardhi kwa ajili ya vijana isipokuwa Mkuu wa Wilaya ya
Dodoma Mjini, Lephy Gembe, ambaye alisema kuwa Sera za Mamlaka ya Ustawishaji
Makao Makuu (CDA) ni kikwazo kwa wilaya yake.
Kwa upande mwingine Chiza alisema ni wakati sasa wa Tanzania
kuondoka katika kilimo cha kujikimu na kwenda katika kilimo cha uzalishaji
zaidi ili kuinua tija.
Alisema Sera yake ni kuzalisha kwa wingi na kutafuta masoko na
si kuzuia mazao ya Tanzania kuvuka kwenda nje ya nchi kama inavyofanyika kwa
sasa.
Akizungumzia gharama za maonyesho ambazo zimekuwa zikilalamikiwa
na wadau, alisema “hatuwezi kufuta maonyesho ya Nanenane kwa kuwa yana umuhimu
wa pekee na faida kwa wakulima wetu.”
Alisema kuwa malalamiko kuwa maonyesho hayo yanagharimu fedha
nyingi si kweli na kama kuna ukweli wa aina yoyote ipo haja ya kuangalia namna
ya kupunguza gharama lakini si kuyaondoa maonyesho hayo. Hata hivyo, aliwaagiza
viongozi kufanya kwa vitendo ili waweze kuendana na kauli mbiu kuliko kutofanya
hivyo na kufanya kauli mbinu hiyo kuwa ni nyimbo za kasuku.
No comments:
Post a Comment