facebook likes

Friday, July 5, 2013

BALOTELLI USO KWA USO NA MESSI.

MSHAMBULIAJI nyota wa kimataifa wa Argentina, Lionel Messi anatarajiwa kukutana uso kwa uso na mshambuliaji wa Italia Mario Balotelli katika mchezo wa kirafiki maalumu kwa ajli ya kumuenzi Pope Francis. Baada ya miezi kadhaa ya majadiliano, Shirikisho la Soka la Italia hatimaye limetangaza kuwa mechi ya kirafiki baina ya nchi hizo mbili itapigwa Agosti 14 mwaka huu katika Uwanja wa Olimpiki uliopo jijini Rome. Shirikisho hilo limedai kuwa wanatarajia Papa Francis ambaye anajulikana kuwa mshabiki mkubwa wa soka, atakuwepo kushuhudia nchi aliyotoka ya Argentina ikipepetana na Italia kwenye mtanange huo. Mara ya mwisho Italia kukwaana na Argentina ilikuwa ni mwaka 2001 jijini Rome katika mchezo wa kirafiki ambapo Argentina walishinda kwa mabao 2-1.

No comments:

COMMENTS

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...