MADEREVA WA LANGALANGA WATISHIA KUGOMA.
MADEREVA wa mashindano
ya magari yaendayo kasi ya langalanga wametishia kususia michuano ya
Grand Prix ya ujerumani itakayofanyika Jumapili ijayo kama kutatokea
matatizo ya kupasuka magurudumu kama ilivyotokea katika mashindano ya
British Grand Prix wiki iliyopita. Chama
cha Madereva wa Langalanga-GPDA kimedai kuwa wanachama wake wameonyesha
wasiwasi kuhusiana na matukio yaliyopita na kama yakijirudia tena
watalazimika kujitoa kwa ajili ya usalama wao. Katika
michuano ya wiki iliyopita madereva sita walipasukiwa na magurudumu
wakati wakiwa katika mwendo kasi wakiwemo Lewis Hamilton wa timu ya
Marcedes, Felipe Massa na Frnando Alonso wa Ferrari, Jean-Eric Vergne wa
Toro Rosso, Esteban Gutierrez wa Sauber na Sergio Perez wa MacLaren. Tayari
kampuni inayosambaza magurudumu ya Pirelli imeshabadilisha aina ya
magurudumu yatakayotumika katika mashindano ya Grand Prix ya Ujerumani
ili kuepusha matatizo yaliyojitokeza wiki iliyopita.
No comments:
Post a Comment