SIYO siri kwamba wapenzi wasio na kificho, Nasibu Abdul ‘Diamond’ na
Penny Mungilwa wana malengo ya kuja kuishi kama mke na mume lakini
maajabu ni namna mwanamuziki huyo alivyopanga sherehe ya ndoa yao iwe
siku ikifika.Nasibu Abdul ‘Diamond’.
Akizungumza hivi karibuni, Diamond alisema kuwa yamekuwepo
maneno ya chinichini kuwa ameshatoa mahari na siku si nyingi ataingia
kwenye maisha ya ndoa ila ukweli ni kwamba kila kitu kinafanyika kwa
umakini na mashabiki watajulishwa hatua kwa hatua.
Diamond.
“Suala la ndoa yangu nalifanya kwa umakini sana, watu wawe na subira
tu ila wanachotakiwa kujua ni kwamba nina plani za kuifanya sherehe ya
ndoa yangu kwenye Uwanja wa Leaders Club, pale Kinondoni na watu
wataingia kwa kiingilio kisichopungua shilingi elfu kumi. Itakuwa ni
ndoa ya Wasafi bana,” alisema Diamond.