facebook likes

Friday, July 5, 2013

TOGO NAO WAKATWA POINT.

SHIRIKISHO la Soka Duniani-FIFA limeikuta Togo na hatia ya kumchezesha mchezaji asiyeruhusiwa katika mechi ya kufuzu michuano ya Kombe la Dunia dhidi ya Cameroon hivyo kuwanyang’anya ushindi na wa kuwapa Cameroon. Uamuzi huo unamaanisha Cameroon ambao walipoteza mchezo huo kwa mabao 2-0 sasa wamepewa ushindi wa mabao 3-0 na wamekwea kileleni mwa msimamo wa kundi I, kwa tofauti ya alama moja na Libya wanaoshika nafasi ya pili huku wakiwa na mchezo mmoja wa kumalizia. FIFA ilitoa adhabu hiyo kwa Togo baada ya kumchezesha Jacques Alexys Romao wakati alikuwa na adhabu ya kutocheza mechi moja baada ya kupata kadi mbili za njano katika mechi mbili walizocheza. Cameroon sasa wamefikisha alama 10 katika mechi tano walizocheza huku wakitarajia kumaliza mechi yao ya mwisho nyumbani dhidi ya Libya September 6 mwaka huu.

No comments:

COMMENTS

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...