Sehemu
ya Magunia ya Dagaa yakiwa yamepangwa vyema ndani ya soko hilo tayari
kwa kusafirishwa sehemu mbalimbali kwa matumizi ya binadamu na mifugo.
Dagaa
'wachafu' wakiwa wameanikwa chini kwa ajili ya kukaushwa.!Globu ya
Jamii pia ilipata nafasi ya kuzugumza na mmoja wa wafanyabishara wa
dagaa,kuhusiana na bei,akaeleza kuwa dagaa wazuri kwa sasa wanauzwa kati
ya elfu 8 mpaka 12 kwa ndoo ya plastiki,"Lakini pia hawa walioanikwa
hapa chini sisi wakazi wa Mwanza huwa hatuli,tunatengeneza maalum kwa
ajili ya kuwauzia watu wenye mifugo,lakini pia kuna baadhi ya
wafanyabiashara kutoka maeneo mbalimbali nje ya jiji la Mwanza wamekuwa
wakija kuwanunua dagaa hawa "wachafu" kwa ajili ya matumizi ya chakula
na kwenda kuwauza huko mikoani ikiwemo jijini dar es salaam kwa bei
yao"alisema mfanyabiashara huyo ambaye hakutaka jina lake litajwe hapa
mtandaoni.
Sehemu ya soko kuu la Kimataifa la Samaki-Kirumba Mwaloni jijini Mwanza kama lionekanavyo mapema leo mchana
Wakina mama wakijishughulisha na biashara yao ya ndizi ndani ya soko kuu la Kimataifa la Samaki-Kirumba Mwaloni jijini Mwanza
Baadhi ya Wafanyabiashara hao wakiwa bize kuwachambua Dagaa wasiofaa na wanaofaa kwa matumizi mbalimbali.
Sehemu ya bango la soko hilo kama lionekanavyo pichani.
No comments:
Post a Comment