Chuo kikuu cha Dodoma
kimethibitisha kwamba Kozi ya lugha ya kichina itaanza kutolewa kwenye
chuo hicho ambapo makamu mkuu wa chuo Profesa Idris Kikula amesema
uamuzi huo umetokana na kukua kwa ushirikiano wa wafanyabiashara wa
China na wafanyabiashara wa Tanzania.
thecitizen.co.tz wameripoti
kwamba Profesa kasema chuo chake kilikua na malengo ya kuandaa walimu
ambao watakua wakifundisha lugha ya kichina kwenye shule za sekondari
Tanzania pamoja na taasisi nyingine za elimu.
Info za uhakika ni kwamba mwaka
2006 wageni kutoka nchi mbalimbali duniani wasiozidi laki mbili
walikwenda China kujifunza kichina, na wakati huohuo watu wapatao
milioni 20 sehemu mbalimbali duniani wameshajifunza lugha ya kichina
No comments:
Post a Comment