TABIA ya kujadiliwa
kwa hoja za Mawaziri wa Elimu, Mafunzo na Ufundi Shukuru Kawambwa, na
wa Maji, Profesa Jumanne Maghembe na hatimae kuungwa mkono na Wabunge wa
Vyama vyao, zimetafsiliwa kama ni Kuwasaliti wananchi waliowapa Kura.
Sababu ya
kutafsilika hivyo, kumetokana na kwamba mara zote zimekuwa zikipendekeza
kuondolewa bungeni kwa hoja binafsi zilizowasilishwa mapema na wabunge
wa upinzani, ambazo wananchi wanaona zina dhima ya Mustakabali wa Taifa.
Hoja binafsi
zilizohasimiwa na mawaziri hao ziondolewe ni pamoja na Udhaifu wa Sekta
ya Elimu iliyowasilishwa na Mbunge wa kuteuliwa James Mbatia-NCCR
Mageuzi, na ya Maji ambayo mapema iliwasilishwa na Mbunge wa Ubungo
(Chadema), John Mnyika.
Kinachopelekea
tafsiri hizo, ni pamoja na Mawazi wa Wizara zingine kutoweka pingamizi
la kuondolewa kwa Hoja binafsi ya Mbunge wa Jimbo la Iramba Magharibi
Mwigulu Nchemba kuhusu mikopo ya Elimu ya Juu.
Hoja
nyingine ni ile ya Mbunge wa Nzega Dk. Hamisi Kigwangala ya mpango
maalumu wa kukuza ajira kwa vijana kwa kuanzisha mfuko wa mikopo
ya vijana wanaowekeza kwenye kilimo na viwanda vyenye uhusiano wa moja
kwa moja na kilimo kwa hoja Mbadala za
Kama
ilivyofanyika kwa Mbatia alipowasilisha Hoja ya Udhaifu wa Sekta ya
Elimu, ndivyo ilivyofanyika kwa Mnyika katika hoja yake aliyokuwa
akitaka Bunge liazimie kuitaka Serikali ichukue hatua za haraka ya
kuboresha upatikanaji wa maji safi na ushughulikiaji wa majitaka katika
Jiji la Dar es Salaam.
Hapa
ndipo nilipoona umuhimu wa wa bunge hili la kichama na kishabiki kuwa
ni kubadilisha utaratibu katika katiba mpya, spika na naibu wake wasiwe
wabunge na wasiwe na chama chochote cha siasa, na mawaziri nao wasiwe
wabunge.
Sikubaliani
kwamba kila kinachoongelewa na upinzani ni cha kubeza, ieleweke kuwa,
ukiyakataa mapendekezo ya upinzani si kana kwamba umewapinga wao bali
unakuwa umewapinga wananchi walioko nyuma yao.
Kilicho
mbele yetu, tunatakiwa tuweke Utaifa kwanza na kasha ndipo vyama vyenu
baadae. Lakini nimehuzunishwa sana na mwenendo wa Bunge letu, ambalo
sasa naona limekuwa halina utaifa kwa baadhi ya wabunge, bali
limegubikwa na uvyama.
Wananchi sasa
tunaamini kwamba, kila inapotolewa hoja ya manufaa kwa wananchi hasa
inapotolewa na wapinzani, Spika au Naibu Spika wa Bunge anaizima, hivyo
kwa tabia na muktadha huo, tunajua wabunge wa chama cha cha mapinduzi
(CCM), wameamua kututesa wananchi , Je. Hawajui mwaka 2015 uko
mlangoni?.
Kiukweli
mpaka sasa, Bunge limewaonesha wananchi kwamba halina maadili, na
lawama zote lazima tuwatupie wasimamizi wa Bunge wakiongozwa na Spika
na Naibu Spika. Lazima ifike mahali wabunge waogope na kuona jinsi
wapiga kura walivyopigwa Jua na Mvua ili kuwafanya wawe wawakilishi wao,
kuliko hivi wanavyoisimamia Serikali kinafiki.
Hivi
wabunge; Je,mmesahau kabisa kwamba kuna watu wanakufa huku na nchi iko
katika hali mbaya kwa njaa,,, migogoro ya kijamii na kidini, elimu haina
mwelekeo wala haimuandai mtanzania kujitegemea zaidi ya kuwa mtumwa wa
ajira
Aidha
najihoji moyoni Je, baadhi yenu mtapataje uchungu kama mishahara yenu
imefikia million tatu nukta sita ukiondoa marupurupu!! Basi kama tatizo
ni siasa,,,Rais Kikwete licha ya juhudi zake zinazosemekana ni
nyingi ili atakapokabidhi kijiti aweze kukumbukwa, Wabunge hawa ndio
watu uliopewa na wananchi ili wakusaidie kutokomeza Umasikini, Ujinga na
Maradhi.
No comments:
Post a Comment