Jumatatu february 4 2013 msanii
Mrisho Mpoto alitangaza kwa mara ya kwanza kupitia AMPLIFAYA ya CLOUDS
FM kwamba mwaka 2015 ataingia kugombea Ubunge kwenye jimbo lolote
Tanzania ambalo mbunge wake analegalega.
Baada ya taarifa yake kusikika
alipokea simu 80 zikiwemo 12 za wanasiasa pamoja na sm 400 kutoka kwa
watu mbalimbali ambao wamempongeza na wengine wakimuuliza maswali huku
wabunge wakiongea nae kuhusu kujiunga nao.
Namkariri akisema “ni wazo
ambalo limetoka kwa wananchi wenyewe wakisema nadhani tumekosea kupeleka
mwakilishi, nadhani mwakilishi wetu ni wewe kwa hiyo ile demand ya
wananchi imekua kubwa, nikasema hapana sasa lazima niende mwenyewe.
Amesema “nimekua mwakilishi wa
wananchi kwa muda mrefu upitia nyimbo zangu lakini watu hawataki kusikia
wala kubadilika, tunapozungumzia maisha tunazungumzia madirisha manne,
kuna dirisha la kwamba wananchi wanajua wewe hujui, la pili mwananchi
anajua wewe hujui, la tatu mwananchi hajui na wewe hujui, la nne wewe
unajua mwananchi anajua kwa hiyo dirisha hili wawakilishi wetu wamekua
wakitumia vibaya sana wanafikiri wananchi hawajui wao ndio wanajua, ile
dhana ya kuona wananchi hawajui ila wao ndio wanajua tunataka
tukaionyeshe, tumezungumza sana” – Mpoto
“Hebu angalia mfano mzuri wa
pale Mtwara, leo mpaka watu wanakufa mtu anasema siwezi kwenda kusaidia
kule kwa sababu mimi mbunge wa jimbo lako, jimbo gani? wewe ni mbunge wa
wananchi, unapokua mbunge ni mbunge wa Watanzania wote, watu hawataki
kushughulika nao mpaka viongozi wanakuja kutoka huko ndio wanakwenda
kule kuzungumza, haya mambo kama yanaweza kuzungumzwa yangetokea? alafu
unasema amekufa mtu mmoja tu watu wawili? ile pia ni roho, ile pia ni
damu, tumeshindwa kusikilizwa hapa tutasikilizwa tukiwa kulekule ndani ”
– Mpoto
Mpoto amesema mpaka sasa anayo
kadi ya chama japo hataki kutaja ni chama gani lakini ahadi yake ni
kwamba ndani ya wiki chache zijazo atatangaza Exclusive kupitia
AMPLIFAYA ni chama gani atakachogombea nacho huku akisisitiza kuwa
wananchi wanahitaji vitu vitano tu ambavyo atavieleza wakati
utakapofika.
No comments:
Post a Comment