News, Events, Entertainment, Sports, Lifestyle, Fashion,politics, Beauty, Inspiration and yes... Gossip!
facebook likes
Wednesday, February 6, 2013
Tundu Lissu hana fujo, kiti cha spika ndio kinapwaya!
Spika wa bunge la jamhuri ya muungano wa Tanzania amemtaja mbunge wa singida mashariki Mhe Tundu Lissu kuwa ni mbunge anae ongoza kwa fujo na msumbufu bungeni! Hii ni mara ya kwanza katika historia ya bunge la jamhuri ya muungano wa Tanzania kumsikia spika wa bunge akitaja orodha ya majina ya wabunge wenye fujo na wasumbufu. Nikiri kuwa sijawahi kumsikia spika yoyote kabla ya mama Makinda akifanya kama alivyo fanya mama huyu!
Baada ya mama Makinda kumtaja Tundu Lissu kuwa ndiye mbunge msumbufu na mwenye fujo kuliko wabunge wote mjengoni, Nimejikuta najiuliza maswali kadhaa.
1. Je ni kweli Tundu Lissu ni mbunge msumbufu na mwenye fujo bungeni kwa maana ya halisi ya usumbufu na fujo?!
2. Je kuzisimamia, kuzifuata na kuzijua kanuni za bunge huku akitaka kiti cha spika kizisimamia na kuzifuata kanuni hizo pale kinapo yumba ndio usumbufu au fujo?
3. Je, ulio itwa usumbufu na fujo za Tundu Lissu bungeni una tija kwa wananchi wanao fuatilia bunge na unawakera wananchi hao au unakikera tu kiti cha spika?
4. Je, kiti cha spika kimeonyesha umahiri wa kiutendaji kwa maana ya utendaji wa haki usio egemea itikadi wala kuegemea chama tawala bila kuwakwaza wananchi na wabunge wa upinzani?
5. Je usumbufu na fujo za Tundu Lissu bungeni na maamuzi ya kiti cha spika ni kipi kina athiri na kuwasumbua watanzania katika mfumo na aina ya bunge tulilo nalo leo?!
MTAZAMO WANGU.
Mimi kama mwananchi wa kawaida ninae fuatilia bunge naona fujo na usumbufu alio batizwa Tundu Lisu unafaa uelekezwe kwenye kiti na mamlaka dhaifu ya spika wa bunge la jamhuri ya muungano wa Tanzania.
Kwa nini?
1. Mpaka sasa kiti cha spika kimeonyesha udhaifu na kimeonekana kuyumba huku kikionyesha upendeleo wa wazi wazi kwa wabunge wa ccm na kukandamiza wabunge wa upinzani. Ushahidi ni yanayoendelea bungeni kuanzia kwenye hoja ya Lema kuhusu waziri mkuu kulidanganya bunge hadi kwenye hoja binafsi za wabunge wa upinzani kuzuiliwa huku za wabunge wa ccm kuruhusiwa kusomwa.
2. Mpaka sasa rufaa 10 za wabunge wa upinzani hasa Chadema hazija patiwa majibu huku wabunge haohao wengi wakitegemewa kuitwa kwenye kamati ya maadili na nidhamu ya bunge kwa kile kilicho itwa kuvunja kanuni za bunge. Jiulize kwa nini ni miaka takribani miwili sasa hakuna rufaa hata moja iliyo jibiwa wakati nyingine zina majibu ya wazi kabisa mfano ile ya Pinda kuongea uwongo bungeni kuhusu mauwaji ya waandamaji wa Chadema mkoani Arusha?
3. Mpaka sasa wabunge wengi wa upinzani ndio wamelalamikia kuonewa na kiti cha spika kuliko wabunge wa ccm. Mara kadhaa hata wanaharakati wameonyesha hisia zao waziwazi kuwa kiti cha spika kina pwaya na kimeonyesha udhaifu wa kiutendaji.
4. Wananchi wengi wa kawaida wameonyesha waziwazi kutokuwa na imani na kiti cha spika kwa jinsi kinavyo endesha bunge. Wana ona kuna tofauti kubwa ya uendashaji wa bunge wa kati wa kipindi cha Mzee Sitta na kipindi hiki cha Anna Makinda.
5. Kuahirishwa kwa bunge hivi karibuni kutokana na ubabe wa kiti cha spika kusababisha vurugu zilizotokea bungeni nao ni ushahidi mwingine kuwa kiti cha spika kina sababisha fujo kutokana na wabunge kutetea haki zao zinazo pokwa na kiti hicho.
HITIMISHO.
Udhaifu na kupwaya kwa kiti cha spika ndio kuna sababisha fujo na vurugu kutokana na kukandimiza upinzani kwa maslahi ya chama tawala na kulinda udhaifu na ombwe la serikali. Tundu Lissu hana fujo na usumbufu unao athiri watanzania kama jinsi maamuzi mabovu ya kiti cha spika yanavyo weza na kuendelea kutuathiri watanzania.
Ulio itwa usumbufu na fujo za Tindu Lissu bungeni hauja zima hoja ya kutekwa na kuteswa kwa Dr Ulimboka wala kuzima hoja za sakata la gesi ya Mtwara, fujo na usumbufu wa Tundu Lissu hauja zima hoja makini ya elimu iliyo tolewa na Mbatia wala hoja ya tatizo la maji ya John Mnyika.
Udhaifu na ombwe la kiti cha spika ndio chanzo cha kumuona Tundu Lissu ni msumbufu kwa kuwa ana kisulubu kiti kusimamia na kuzifuata kanuni.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment