facebook likes

Saturday, July 27, 2013

WAKAGUZI WA MAHESABU WAPONGEZWA NEW YORK MAREKANI


Na Joseph Msami wa Radio ya Umoja wa Mataifa
Mapema wiki hii wajumbe wa bodi ya ukaguzi wa Umoja wa Mataifa walikutana mjini New York Marekani ambapo pamoja na mambo mengine walitia saini ripoti za ukaguzi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa kwa mwaka wa fedha 2012. Miongoni mwa wajumbe hao ni Ludovick Uttouh, Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa hesabu za serikali yaTanzania ambaye aliwakusanya wakaguzi wa mahesabu kutoka Tanzania na wafanyakazi kadhaa wa ubalozi wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa hapa New York kwa hafla wima (cocktail party).
Lengo la hafla hii ilokuwa kuwapongeza wakaguzi kwa kazi nzuri na pia kushukuru ubalozi kwa ushirikiano walioutoa.

Pichani kulia ni  mkaguzi na mdhibiti mkuu wa hesabu za serikali Ludovick Utoh akiongea  wakati wa hafla hiyo.Aliyeko naye hapo pembeni ni mwakilishi wa kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa Balozi Tuvako Manongi.

Chanzo:Swahili Tv

No comments:

COMMENTS

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...