KLABU ya Arsenal imeondoka Mashariki ya
Mbali leo kwa ushindi wa asilimia 100 kwenye mechi zao za kujiandaa na
msimu baada ya kupata ushindi mwembamba dhidi ya Urawa Red Diamonds.
Kinda Chuba Akpom amempa ushindi wa 2-1 kocha Arsene Wenger katika mechi yake ya mwisho kwenye ziara ya Asia.
Jack Wilshere alianza kwa mara ya kwanza
kikosini The Gunners tangu afanyiwe upasuaji wa kifundo cha mguu Mei,
wakati Laurent Koscielny aliyeumia kifundo katika ushindi wa 3-1 dhidi
ya Nagoya Grampus, alianza leo Saitama.
Mabao ya Arsenal leo yamefungwa na Lukas Podolski dakika ya 48 na Akpom dakika ya 82, wakati la wenyeji lilifungwa na Abe dakika ya 58.
Kikosi cha Arsenal kilikuwa: Fabianski;
Sagna Koscielny, Mertesacker/Jenkinson dk46, Miquel; Arteta/Rosicky
dk46, Wilshere/Ramsey dk46, Oxlade-Chamberlain/Zelalem dk67,
Walcott/Akpom dk75, Gnabry/Miyaichi dk46, Giroud/Podolski dk46.
Urawa Reds: Yamagishi; Tsuboi, Nasu, Abe, Ugajin; Kojima, Kashiwagi, Umesaki, Richardes; Yamada na Koroki Subs.

Lukas Podolski (kushoto) alifunga bao la kwanza kwa Arsenal dhidi ya Red Diamonds

Chuba Akpom akishangilia bao lake la ushindi

Yuki Abe na Theo Walcott

Mashabiki wakionyesha sapoti kwa kocha Arsene Wenger mjini Saitama


Olivier Giroud (kushoto) na Serge Gnabry (kulia)

Sapoti kwa Walcott kutoka kwa mashabiki

Mashabiki wa Arsenal Japan wakifurahia mechi leo

Wachezaji wa Arsenal wakionyesha bango baada yA mechi
No comments:
Post a Comment