Kushilla Thomas, Mkurugenzi wa Masoko wa Tanzania Breweries Limited
(TBL) nje ya ofisi za FC Barcelona huko Catalonia Hispania leo hii
baada ya kutangazwa kwa udhamini wa Castle Lager kwa Barcelona. |
Bia ya Castle Lager imeingia makubaliano ya kuidhamini moja
ya klabu maarufu zaidi duniani ya FC Barcelona ya Hispania kwa kipindi
cha miaka mitatu udhamini utakaokifanya kinywaji hicho kuwa bia rasmi ya
FC Barcelona barani Afrika.
Klabu ya FC Barcelona pia imempa zawadi ya Raisi Jakaya Kikwete kwa kutambua mchango wake kwenye maendeleo ya soka nchini |
Ushirikiano huu, uliyosainiwa kwenye
uwanja wa klabu Camp Nou, unaifanya CASTLE Lager kuwa bia rasmi
itakayotumika kwa shughuli yoyote ambayo Barcelona itashiriki kwenye
bara la Afrika na pia itafungua milango kwa mashabiki wa Barcelona
Afrika kuwa karibu na wachezaji wa Barcelona, vifaa, na kumbukumbu. Pia
kupata nafasi ya kusafiri kwenda Hispania kushuhudia kwa karibu timu ya
Barcelona.
Mkataba huu utakuwa
maalum kwa ajili ya CASTLE Lager kwenye nchi nyingi za Afrika isipokuwa
kwa baadhi ya nchi chache zilizochaguliwa ambapo itatumika Castle Milk
Stout.
Hii ni mara ya kwanza kwa timu ya FC
Barcelona kusaini mkataba wa udhamini na kampuni ya bara la Afrika.
Kushirikiana na bia bingwa Afrika litaongeza kwa haraka umaarufu wa timu
ya FC Barcelona ndani ya bara la Afrika na kufungua milango kwa
mashabiki wa klabu hii kupata bidhaa mbalimbali za Barcelona na nafasi
za kushinda safari ya kwenda Barcelona kuitembelea klabu hiyo.
Wawakilishi wa SABMiller kutoka nchi mbalimbali barani Afrika wakiwa nje ya ofisi ya FC Barcelona uko Catalonia Hispania leo hii |
“Tumefurahi sana kuingia katika
ushirikiano na Castle Lager na Castle Milk Stout, chapa zinayofahamika
dunia nzima . Tunafanana na Castle kwa kuwa sote tuna historia ya zaidi
ya miaka 100 na utamaduni uliotukuka. Na sote tuna mapenzi na mpira wa
miguu pamoja na mashabiki wake katika soko muhimu kama Afrika,” alisema
Javier Faus, Makamu wa Rais wa FC Barcelona anayeshughulikia masuala ya
uchumi.
Mkurugenzi wa Masoko wa TBL, Kushilla Thomas akimkabidhi zawadi ya asili kutoka Tanzania Bw. Javier Faus, Makamu wa Rais wa FC Barcelona anayeshughulikia uchumi huko Catalonia Hispania leo hii baada ya kutangazwa kwa udhamini wa Castle Lager kwa Barcelona. |
“Uamuzi wa Barcelona
kuingia ushirika na na bia inayoongoza barani Afrika kutaongeza umaarufu
wa bia hiyo kwenye bara hili na kuwawezesha wachezaji wa timu hiyo
kufika maeneo amabyo hawajawahi kufika barani Afrika,” alisema David Carruthers Mkurugenzi wa Masoko wa SabMiller Afrika (kampuni mama ya TBL).
CASTLE Lager si bidhaa mpya kwenye
udhamini wa mpira wa miguu na vyama, ina miaka mingi ya kujihusisha
katika soka barani Afrika kwa kipindi cha miaka 85 kupitia ligi
mbalimbali za nchi tofauti kama vile Zimbabwe, Swaziland, Botswana,
Lesotho na pia mashindano ya kanda kama COSAFA Kusini mwa Afrika na
CECAFA Afrika Mashariki.
Kutokana na soka la Ulaya kupata
umaarufu mkubwa na mashabiki wengi barani Afrika, Castle Lager imekuwa
ikidhamini urushaji wa matangazo ya ligi hizo kwenye televisheni barani
Afrikana kuwapa mashabiki fursa ya kufatilia kila kinachoendelea kwenye
ligi hizo maarufu duniani ambazo ni Ligi Kuu ya Ulaya, Ligi Kuu ya
Uingereza na La Liga ya Kihispania.
No comments:
Post a Comment