Victor
Wanyama ameondoka Celtic Football Club na kujiunga na klabu
inayoshiriki kwenye ligi kuu ya England - Southampto baada ya
kukamilisha uhamisho wa wa £12.5million. Sasa ikiwa ni wiki kadhaa tangu
kiungo huyo wa Kenya kuondoka, kocha wa Celtic Neil Lennon, amesema
Wanyama alikuwa ndio kiungo wake bora wa ushambuliaji kwenye timu yake
na sasa wanahitaji mbadala wake.
Kutokana
na hilo sasa zimeibuka taarifa kwamba kocha huyo ambaye ni nahodha wa
zamani wa Celtic anamuwania kiungo mwingine kutoka Kenya Humphrey Mieno.
Mieno ambaye kwa sasa ni mchezaji wa Azam FC inayoshiriki kwenye ligi
kuu ya Tanzania.
Celtic,
itabidi ifanye haraka kumsaini mchezaji huyo wa Azam FC kwa kuwa kuna
vilabu vingi barani Afrika kama miamba ya soka ya Tunisia Esperance na
Club Africain zinamuwania kwa nguvu mchezaji huyo ambaye alihamia Azam
akitokea Sofapaka ya Kenya.
Mpaka sasa sio Celtic wala Azam FC ambazo zimethibitisha kuhusu taarifa hizi.
No comments:
Post a Comment