facebook likes

Saturday, July 27, 2013

Liverpool yakaribia kuuzwa.


Kikosi cha Liverpool .

Kikosi cha Liverpool .
Siku chache baada ya kukaribia kumuuza nyota wake Luis Suarez wamiliki wa klabu ya Liverpool ambao ni kampuni ya Fenway Sports Group wako mbioni kuiuza klabu hiyo.
Kampuni hiyo yenye maskani yake huko Boston nchini Marekani ambayo inaongozwa na mfanyabiashara John W Henry iliinunua klabu ya Liverpool toka kwa wafanyabiashara George Gillett na Tom Hicks huku wakiwa na mtazamo wa kibiashara wa kutengeneza fedha kupitia klabu hiyo jambo ambalo halijatokea katika kipindi cha miaka minne ya umiliki wao.
John W Henry aliinunua Liverpool kwa paundi milioni 300 na anataka kuiuza kwa paundi milioni 350. Kwa mujibu wa taarifa toka benki moja ya huko Marekani klabu hiyo imewekwa sokoni kwa mtu yoyote atakayekuwa tayari kuinunua .
Henry anaonekana kuchoshwa na kitendo cha kutotimia kwa malengo ya kibiashara aliyokuwa ameiwekea Liverpool ambapo katika kipindi cha miaka minne klabu hiyo bado imeshindwa kushiriki ligi ya mabingwa na haijaweza kuwa na ubora wa kuwania ubngwa wa ligi ya England .
image
Pamoja na hayo Liverpool pia imekuwa ikipata hasara kwenye soko la wachezaji ambapo mara kadhaa imekuwa ikishindwa kurudisha thamani ya fedha zinazotumika kwenye matokeo uwanjani na hata kwenye mauzo ya wachezaji . Moja ya hasara kubwa ambazo zimemkera mmiliki John W Henry ni kitendo cha kununuliwa kwa Andy Caroll kwa paundi milioni 35 kabla ya kumuuza kwa paundi milioni 19 huku akiwa hajawahi kufanya vizuri kulingana na thamani ya fedha iliyotumika kumsajili.
Uongozi wa Fenway Sports Group ulikutana na kampuni ya mafuta ya Saudi Aramco ya huko Saudi Arabia kujadiliana uwezekano wa kampuni hiyo ya mafuta kuidhamini Liverpool lakini vingozi wa Saudi walikuja na wazo la kuinunua kabisa klabu hiyo . Hadi sasa kampuni mbili zinazomilikiwa na mabilionea wa kimarekani zimeripotiwa kuwa na wazo la kununua Liverpool lakini hakujakuwa na ofa rasmi.

No comments:

COMMENTS

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...