facebook likes

Wednesday, July 24, 2013

Dogo Janja amenunua usafiri huu, ni kwa ajili ya kwendea Shule

Rapper mwenye umri mdogo zaidi TZ, Dogo Janja amenunua usafiri wake wa kwanza kwa pesa za kitanzania Tsh 1.2 Million, ni Pikipiki ambayo mwenyewe anasema atakua anaitumia kwa ajili  ya kwendea shule.

Baada ya kushindwa kufanya vizuri alipokua Makongo High School kwa kushindwa kufikia wastani wa kumuwezesha kuingia form 3, Mkali huyo wa Ya Moyoni sasa amejiunga na Mbezi High School.

Dogo Janja amesema usafiri huo ameununua kutokana na kukichanga baada ya kufanya Shows, na amekiri kwamba Pikipiki hiyo amenunua kwa mtu kwa bei ya Tsh 1.2 Mil., 
Dogo Janja anatarajia kuachia ngoma mpya itakayoitwa Serebuka ambao ameufanya kwenye studio za Noizmekah huko Arusha. Producer ni DX na wimbo huo amewashirikisha Jambo Squad.

No comments:

COMMENTS

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...