facebook likes

Wednesday, July 24, 2013

PAMOJA NA KUCHUKUA UBINGWA - BAYERN YAPOTEZWA KWENYE KUINGIZA FEDHA NYINGI NA JUVE KWENYE LIGI YA MABINGWA - MAN UNITED YAONGOZA ENGLAND,



Juventus wanaweza wakawa wametolewa kwenye robo fainali lakini ndio timu iliyopata mapato makubwa kutoka kwenye michuano ya ubingwa wa ulaya msimu uliopita.

Bayern Munich iliwafunga wapinzani wao wa Ujerumani Borussia Dortmund 2-1 katika fainali ya mabingwa wa ulaya katika uwanja wa Wembley mwezi Mei, lakini hakuna yoyote katika timu hizo zilizocheza fainali ambayo imeifikia Juventus kimapato.

Mabingwa wa Italia wameingiza kiasi cha €65.3 million kutoka kwenye ligi ya mabingwa msimu uliopita, €10 million zaidi kuliko Bayern Munich.
Dortmund wamefuatia kwa kutengeneza kiasi cha €54.2 million.
Vilabu 32 vilivyoshiriki katika hatua ya makundi vimegawana kiasi cha €904.6 million, kwa mujibu wa Uefa.
Tofauti kubwa iliyopo baina ya miamba iliyocheza fainali na Juve ilikuwa ni haki za matangazo ya TV, kwa wataliano wa Turin wakiingiza kiasi cha €44.8 million kupitia haki za matangazo ya TV, ukilinganisha na €19.1 million walichoingiza Bayern.

AC Milan, ambao waliweza kuingia raundi ya pili tu, wenyewe waliingiza kiasi cha €51.4 million mbele ya miamba ya Hispania Real Madrid (48.4m) na Barcelona (45.5m) miamba ya Ufaransa  Paris Saint-Germain (44.7m).
Pamoja na kufanya vibaya kwenye michuano hiyo lakini pia timu za England safari hii zimeshuka sana kwenye kuingiza fedha nyingi - mabingwa wa nchi hiyo Manchester United ndio wamewaongoza wenzao kwa kuingiza €35.6 million.

Timu ambayo imeingiza fedha kidogo kabisa ilikuwa ni Dynamo Zagreb waliingiza kiasi cha €10.5 million.

No comments:

COMMENTS

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...