facebook likes

Wednesday, July 24, 2013

Bosi wa Liverpool awabeza Arsenal.


Mmiliki wa klabu ya Liverpool John W Henry amewabeza viongozi wa Arsenal kwa kuwauliza ni kitu walichovuta ambacho kimewapa mawazo kuwa wanaweza kumsajili mshambuliaji Luis Suarez toka Liverpool.

Luis Suarez.
Luis Suarez.
John W Henry kwa kauli hiyo ameonekana kama amemaanisha kuwa labda Arsenal wametumia madawa ya kulevya yanayowachanganya mpaka kufikiri kuwa Liverpool inaweza kumuachia mchezaji huyo .
Mmiliki huyo ametoa kauli hiyo kupitia ukurasa wake kwenye mtandao wa kijamii wa twitter na maneno yake yalisomeka hivi “What do you think they’re smoking over there at Emirates? akimaanisha kuwa “Unadhani ni kitu gani wanachovuta pale Arsenal”
image
Arsenal wamepeleka ofa mbili za kujaribu kumnunua Luis Suarez huku Liverpool ikizikataa ofa zote mbili .
Suarez aliwasili nchini Australia juzi na ataichezea liverpool kwenye mechi ya kirafiki hii leo.

No comments:

COMMENTS

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...