Wakati bajaj zinaanza kufanya kazi kulikuwa
na ugomvi kati ya taxi na bajaj kwasababu ya kile kilichodaiwa kwamba
ni kuchukuliana wateja hadi pale serikali ilipowatambua madereva bajaj
kwa kuanza kulipa kodi. Hivi sasa kuna kampuni ya wachina ambayo
imeingiza aina mpya ya bajaj tofauti na zilizoeleka hapa Dar na
kwingineko. Bajaj za kawaida zinauwezo wa kubeba abiria watatu tu nyuma
na kama abilia ana mzigo itabidi aubebe mwenyewe. Hii bajaj mpya
inauwezo wa kubeba abilia watano nyuma na
wakakaa vizuri bila shida. Kiti cha mbele kinabeba watu wawili hivyo
kuongeza idadi ya abilia hadi sita. Kitu kingine kizuri ni kwamba kuna
sehemu maalum kabisa ya kuwekea mizigo ya abilia na bajaj ikatembea bila
hata watu wengine kujua kwamba kuna mizigo imebebwa. Watu wa sokoni hii
kitu wataifurahia zaidi kwasababu ya hii sehemu ya kuwekea mizigo yao
wakitoka kununua.
Unaambiwa ukinunu moja ni milioni 6.5,
ukinunua mbili kila moja ni millioni 6.4 na ukinunua kumi kila moja ni
millioni 6.1. Zinapatikana Dar hivi sasa. Engine yake ni 150cc.
Lakini pia unazikumbuka hizi bajaj, zilikuwepo kadhaa ndani ya Dar es
salaam chache sana kwa ajili ya promosheni ya Vodacom kipindi flani
kilichopita lakini hazikuwa zinauzwa kubeba abiria.source:millardayo
No comments:
Post a Comment