facebook likes

Wednesday, July 24, 2013

BEYONCE AUMBUKA BAADA YA NYWELE ZAKE KUNASWA NA FENI AKIWA KATIKA SHOW HUKO CANADA



Jumatatu usiku (July 22) Beyonce alikuwa na show huko Montreal, Canada...

Wakati anaimba wimbo wake wa ‘Hallo’ ghafla  nywele zake zikanaswa na feni iliyokuwa nyuma yake jukwaani hapo, nina uhakika kwa msanii mwingine angeweza hata kupoteza mwelekeo na huenda ingemharibia show..

Lakini uzoefu na kujiamini vilimsaidia Bey mama wa mtoto mmoja (Blue Ivy) ambaye hakutetereka na aliendelea kuimba bila hata kupoteza mstari wala kutoka nje ya beat (Ki professional zaidi).

Bey alisimama kwa muda huku wasaidizi wake wakijaribu kukata sehemu ndogo ya nywele zake na mkasi ili aweze kuwa huru na kuendelea na show. Zoezi lilifanikiwa na kipenzi cha Jigga aliendeleza makamuzi.

No comments:

COMMENTS

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...