facebook likes

Wednesday, July 24, 2013

BREAKING NEWS! BEKI WA BLACK LEOPARDS VINCENT MABUSELA ATUA NCHINI KUJIUNGA NA SIMBA



Ikiwa zimebakia siku chache kabla ya kufungwa kwa dirisha la usajili kwa vilabu vya ligi kuu nchini,Timu ya Simba imempokea beki raia wa Afrika ya kusini Vincent Mabusela kwa kwa ajili ya kujiunga na timu hiyo kwa msimu ujao.
Beki huyo ambaye anatokea klabu ya Black Leopards ambayo imeshuka  daraja msimu uliopita katika Ligi kuu nchini humo,amepokewa jioni hii katika Uwanja wa Ndege wa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere na Mjumbe wa Kamati ya utendaji ya Klabu ya Simba Daniel Manembe.


source:shaffihdauda 

No comments:

COMMENTS

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...