facebook likes

Sunday, August 11, 2013

TANZANIA YAZIDI KUPOROMOKA VIWANGO FIFA.


TANZANIA imezidi kuporomoka katika viwango vya ubora vya Shirikisho la Soka Duniani-FIFA ambavyo hutolewa kila mwezi. 
...SOMA ZAIDI....
Mwezi Juni mwaka huu Tanzania ilikwea mpaka nafasi ya 109 hivyo kuleta matumaini lakini hali hiyo ilitoweka baada ya mwezi uliopita kuporomoka mpaka nafasi ya 121 na mwezi huu kuendelea kushuka zaidi kwa nafasi saba mpaka nafasi ya 128. Kwa upande wa Afrika Ivory Coast imeendelea kutamba katika nafasi ya 13 duniani wakifuatiwa na Ghana waliopo katika nafasi ya 24 huku Mali wao wakiwa katika nafasi ya tatu kwa kushika nafasi ya 28 duniani. Nafasi ya nne inashikiliwa na Algeria ambao wako katika nafasi ya 34 na mabingwa wa soka Afrika Nigeria wao ndio wanafunga orodha ya tano kwa Afrika baada ya kushika nafasi ya 35 katika orodha za dunia. Kwa upande wa orodha hizo dunia hakuna mabadiliko yaliyotokea ukilinganisha na mwezi uliopita ambapo Hispania wameendelea kukaa kileleni wakifuatiwa na Ujerumani katika nafasi ya pili huku nafasi ya tatu ikishikiliwa na Colombia, Argentina wanne na Uholanzi wako katika nafasi ya tano.

No comments:

COMMENTS

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...