facebook likes

Sunday, August 11, 2013

MOYES SASA AHAMISHIA MAWINDO KWA LUKA MODRIC BAADA YA KUCHEMSHA KWA FABREGAS

KOCHA David Moyes sasa amehamishia mawindo yake kwa Luka Modric baada ya kukwama kumsajili kiungo wa Barcelona, Cesc Fabregas.Luka who United: Modric is now a target for United boss Moyes after failing to lure Fabregas
...SOMA ZAIDI......Kocha huyo wa Manchester United amemuorodhesha kiungo huyo wa Real Madrid katika orodha ya wachezaji wa kusajili. 
Modric, mwenye umri wa miaka 27, amekuwa akitakiwa na United tangu enzi za Sir Alex Ferguson ambaye alizidiwa kete na Real Madrid mwaka uliopita.
Luka anayetakiwa United: Modric sasa anatakiwa na kocha wa United, Moyes baada ya kushindwa kumpata Fabregas

Alijiunga na Madrid kutoka Tottenham kwa dau la Pauni Milioni 33 ingawa ameshindwa kung'ara La Liga na mashabiki wa timu hiyo wamempigia kura katika wachezaji wa ovyo waliosajiliwa msimu uliopita.
Pamoja na hayo, kocha Jose Mourinho alimtetea wakati wa maandalizi ya msimu kabla ya Modric kuisaidia Madrid katika Ligi ya Mabingwa wakiifunga United Uwanja wa Old Trafford.
Moyes pia anawataka wachezaji wa Everton, Marouane Fellaini na Leighton Baines, lakini inafahamika hayatakuwa majina makubwa yatakayofurahisha mashabiki wa United.
Wanted man: The new United boss had tried to sign Fabregas, but the Barca star decide to stay in Spain
Wanted man: The new United boss had tried to sign Fabregas, but the Barca star decide to stay in Spain
Anatakiwa: Kocha mpya wa United amepambana sana kuwania saini ya Fabregas, lakini nyota huyo Barca ameamua kubaki Hispania

No comments:

COMMENTS

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...