USHINDI wa mabao 3-1 ambao Arsenal
imeupata kwenye Uwanja wa Olimpiki mjini Helsinki dhidi ya
Manchester City katika mchezo wa kirafiki unamaanisha The Gunners
wanaweza kuendelea na maisha bila Luis Suarez.

Arsene Wenger anahaha kusaka saini ya
mshambuliaji huyo asiyefurahia maisha Liverpool akiwa ana matumaini
makubwa ya kumpata Suarez, licha ya ofa yake ya Pauni Milioni 40 kupigwa
chini.
Katika mchezo wa leo, mabao ya Arsenal yamefungwa na Theo Walcott dakika ya tisa, Aaron Ramsey dakika ya 59 na Olivier Giroud dakika ya 62, wakati bao la City limefungwa na Negredo dakika ya 80.
Kikosi cha Arsenal kilikuwa: Szczesny/Fabianski
dk46, Sagna/Jenkinson dk73, Mertesacker, Koscielny, Gibbs, Arteta/Perez
dk68, Ramsey/Hayden dk88, Wilshere/Cazorla dk46, Podolski/Giroud dk46,
Oxlade-Chamberlain/Zelalem dk74 na Walcott
Manchester City: Hart,
Zabaleta (Richards 46), Kompany, Lescott/Boyata dk86, Clichy,
Milner/Navas dk46, Fernandinho/Rodwell dk80, Toure/Garcia dk68, Silva,
Negredo/Jovetic dk68 na Dzeko/Nasri dk46.

Mashabiki wa Arsenal

Yaya Toure akipambana na Aaron Ramsey

David Silva (kulia) na Mikel Arteta wakigombea mpira

Theo Walcott akimtungua Joe Hart kuifungia Arsenal bao la kwanza

Pablo Zabaleta na Alex Oxlade-Chamberlain (kulia) wakipambana

Vincent Kompany akijiandaa kuanzisha mashambulizi

Tayari? Mashabiki wa Arsenal wakitamba na bendera ya Finland mjini Helsinki kabla ya mechi

Carl Jenkinson akipambana na Samir Nasri

Kilaini namna hiyo: Aaron Ramsey akimtungua kipa Joe Hart

Amepagawa: Kiungo wa City, David Silva aliudhiwa na uamuzi wa refa kipindi cha kwanza

Walcott ameifungia Arsenal leo
No comments:
Post a Comment