Waziri
wa Mashauri ya Kigeni wa Rwanda amesema kamwe hawatawafukuza Watanzania
wanaoingia na kutoka nchini Rwanda kwa shughuli mbalimbali kwani tupo
ndani ya shirikisho la Afrika Mashariki na hata kihistoria Rwanda
haijawahi kuwa na tatizo na Tanzania.
.....SOMA ZAIDI...Akizungumzia sakata la
wahamiaji haramu wa Kinyarwanda kufukuzwa na serikali ya Tanzania
amesema, kila nchi inayo mamlaka ya kufanya vile inafaa lakini ingekuwa
vizuri Tanzania ingewasiliana na Rwanda ili kujua wataondokaje na
kupokelewa vipi.
Amesisitiza, "Kwa kuwa wenzetu wameamua kufanya hivyo, tupo tayari kuwapokea wananchi wetu" Lakini pia, Waziri huyo amesema waasi wa FDRL ni kikundi cha wauaji wanaojipanga kuangamiza watu fulani nchini Rwanda hivyo wanatakiwa kupingwa kwa nguvu zote badala ya kuwatambua na kuzungumza nao kama kundi halali na lenye nia njema.
Naye Mtanzania Mohammed, amependekeza Rais Kagame na Kikwete wakutane na kufikia suluhu.Pia baadhi ya Wanyarwanda wamelalamikia kutokutendewa haki kwa kutenganishwa na wake,waume, n.k

No comments:
Post a Comment