facebook likes

Sunday, August 11, 2013

SERENA WILLIAMS ATAKATA TORONTO.


MWANADADA nyota katika tenisi wa Marekani, Serena Williams amefanikiwa kutinga hatua ya robo fainali ya michuano ya Kombe la Rogers kwa kumgaragaza Kirsten Flipkens wa Ubelgiji. 
..SOMA ZAIDI....Williams ambaye anashika namba moja katika orodha za ubora wa mchezo huo duniani kwa upande wa wanawake alimfunga Flipkens ambaye anashika namba 13 katika orodha hizo kwa 6-0 6-3 na sasa anatarajiwa kuchuana na Magdalena Rybarikova. Rybarikova mbaye ni raia wa Slovakia alitinga hatua hiyo baada ya kumchapa Marion Bartoli kwa 7-6 1-0 mchezo ambao haumalizika baada ya Bartoli kujitoa baada ya kuumia mgongo. Kwa upande mwingine wanadada Agnieszka Radwanska, Li Na na Sara Errani nao pia walisonga mbele baada ya kushinda mechi zao wakati kwa upande wa wanaume bingwa wa michuano ya Wimbledon Andy Murray alijikuta katika wakati mgumu baada ya kupokea kichapo cha kwanza toka Mei kutoka kwa Ernests Gulbis.

No comments:

COMMENTS

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...