facebook likes

Sunday, August 11, 2013

BAYERN YAANZA MSIMU KWA USHINDI.


MABINGWA wa Bundesliga, Bayern Munich jana wameanza vyema kutetea taji lao hilo kwa ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Borussia Moenchengladbach na kuchukua alama zote tatu katika mchezo huo wa kwanza wa msimu. 
..SOMA ZAIDI.....Mabao yaliyofungwa na Arjen Robben na Mario Mandzukic katika kipindi cha kwanza na lingine la penati la David Alaba katika dakika ya 69 yalitosha kuwatumia ujumbe wapinzani wao kwamba wamepania kutetea taji hilo msimu huu. Akihojiwa mara baada ya mchezo huo Guardiola amedai kuwa kikosi chake kinahitaji matokeo kama hayo ili kujenga kujiamini zaidi kwasababu wachezaji bado hawajazoea kucheza mechi nyingi. Guardiola ambaye alichukua nafasi ya Jupp Heynckes mwishoni mwa msimu uliopita alitumia wachezaji 10 kati ya 11 ambao waliifunga Borussia Dortmund katika mchezo wa fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya Mei mwaka huu.

No comments:

COMMENTS

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...