facebook likes

Wednesday, August 7, 2013

REAL MADRID YAICHAPA BARCELONA 9 KWA TANO

Legends: Can you name the ten former Barcelona and Real Madrid legends?NYOTA wa zamani wa Real Madrid na Barcelona....SOMA ZAIDI...
wamemenyana katika soka ya wachezaji watano watano maarufu Futsal kwenye michuano ya Kuwait, na Madrid wamewafumua wapinzani wao.
Michael Owen alikuwa miongoni mwa wachezaji walioiongoza Real kuofumua Barca katika michuano ya Al Roudan mabao 9-5.
Na Owen alikuwa mwenye furaha kwa ushindi wa timu yake, baada ya kupata ushindi wa jumla mara mbili na kufungwa mara moja katika El Clasicos: "Tukiwa tumeshinda mechi moja na kufungwa moja, leo ilikuwa mechi ya kuamua mshindi wa jumla! Real Madrid 9 Barcelona 5. #boom," 
VIDEO Mabao yote ya mechi za El Clasico Kuwait.

Magwiji: Unaweza kutaja majina ya wachezaji hawa magwiji wa zamani wa Barcelona na Real Madrid?
Timu ziliunda vikosi vyha magwiji wake kutoka Madrid na Barcelona waliowika miaka ya nyuma. Kulikuwa kuna wachezaji wa England pande zote, huku timu sita zikiwa zilizocheza Ligi Kuu England.
Kwa Real Madrid, Bodo Illgner alikuwa langoni, shujaa wa zamani wa Bolton, Fernando Hierro, Luis Figo, Owen na mshambuliaji wa zamani wa Liverpool, Fernando Morientes. 
Walipambana na Vitor Baia aliyesimama milingotini, beki wa zamani wa Chelsea, Juliano Belletti, Gianluca Zambrotta, kiungo wa zamani wa Middlesbrough, Gaizka Mendieta na mshambuliaji wa zamani wa Newcastle, Patrick Kluivert. 
Kulikuwa pia kuna wachezaji kadhaa wa Futsal kutoka Kuwait katika michuano hiyo.
Timu hizo zilitoka sare ya 4-4, kabla ya Madrid kucharuka na kufunga mabao zaidi yaliyowapa ushindi huo.
Belletti alifunga Hat-trick - mawili akifungia kutokea kwenye nusu yao - wakati Owen alifunga moja, akipasua katikati ya mabeki wawili kabla ya kumtungua kipa hodari wa Ureno.
Morientes pia alifunga Hat-trck, wakati Figo, Hierro na Mendieta walifunga pia nao.

No comments:

COMMENTS

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...