facebook likes

Wednesday, August 7, 2013

MUUZA KAHAWA ASHINDA MILIONI 1 ZA WAZO BORA LA KUTWEETS NA MENGI


Hongera kwa kushika nafasi ya kwanza.
....SOMA ZAIDI.....
http://2.bp.blogspot.com/-OlpTOsNZjTY/UgFt--C-5MI/AAAAAAACY0M/mrFHLKAusuo/s640/Pg.2.JPG
  Mwenyekiti wa Kampuni za IPP, Dk. Reginald Mengi akimkabidhi zawadi mshindi wa kwanza wa shindano la wazo bora juu ya kujikwamua kiuchumi ‘Kutweets na Mengi’, Tony Alfred katika hafla hiyo ilifanyika jijini Dar es Salaam Jana.
 Washindi wakiwa katika picha ya pamoja na Mwenyekiti wa Kampuni za IPP, Dk. Reginald Mengi (kulia).
 
MWENYEKITI wa Kampuni za IPP, Dk. Reginald Mengi, amesema vijana wanaosubiri mifumo iliyowekwa iwasaidie kujikwamua kiuchumi wataendelea kubaki kuwa watumwa wa maamuzi ya watu wengine.
Mengi alitoa kauli hiyo jijini Dar esSalaam, wakati akikabidhi zawadi kwa washindi watatu walioshinda shindano la wazo bora la 'kutweets na Mengi'.
Amesema kwa sasa vijana wengi wanamaliza elimu ya msingi Sekondari na vyuo vikuu ambao hawana ajira wala mitaji na wengi wao wanajisikia kama hawana pa kutokea.
Aliongeza kuwa licha ya serikali, jamii na wazazi kuwa na wajibu katika jambo hili kijana anapaswa kuwa mtu wa kwanza kutafuta njia inayowezekana kwake.
Swali la mwezi Julai lililowatoa washindi hao liliuliza “Kijana asiyekuwa na ajira wala fedha anawezaje kuanza kujijenga kiuchumi” ambapo Tony Alfred muuza kahawa katika kituo cha mabasi Ubungo aliibuka mshindi  wa kwanza.
Alfred ambaye ni msomi wa shahada ya masoko kutoka chuo kikuu cha Dar es Salaam, aliwashinda John Mkungu na Maduhu Jumanne kwa jibu lake lililoeleza kuwa “kama kijana fikiria katika hali uliyopo ni nini unachoweza kufanyia jamii yako, ukipata jibu huo ndio mtaji na ajira yako.”
Kutokana na ushindi huo Alfred amejipatia Sh Mil 1 ambapo John Mkungu alishika nafasi ya pili na kujipatia kiasi cha Sh laki 5 na  maduhu Jumanne alijipatia sh. laki 3.
Mengi aliongeza kuwa kutokana na watu wengi kuchangia katika mtandao wake wa kijamii wa Tweeter, ataanda mpango wa kuyakusanya mawazo yaliyokuwa mazuri na kuyaweka katika mfumo sahihi kisha kuyafikisha kwa vijana wengine kupitia mashuleni na vyuoni.
Akizungumzia ushindi wake, Alfred alimshukuru Mengi kuanzisha mfumo huo na kuwataka vijana wenzake wasikate tamaa pale wanapokosa ajira za serikali.

No comments:

COMMENTS

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...