facebook likes

Wednesday, August 7, 2013

DIAMOND AKWAMA KENYA BAADA YA KUZUKA MOTO, ALIKUA ANATOKA AFRIKA KUSINI

Tukio la moto lililotokea leo alfajiri kwenye uwanja wa kimataifa wa Jomo Kenyatta, JKIA jijini Nairobi Kenya, limemsababisha Bongo Flava Prince, Diamond Platnumz kushindwa kurejea nchini katika muda aliokuwa amepanga.
IMG-20130807-WA0002 
....soma zaidi.....
Diamond akionekana mwenye uchovu mkali akiwa kwenye basi lililobeba abiria kwenda hotelini, pembeni yake ni dancer wake Moses Iyobo
Diamond na abiria wengine waliokuwa wasafiri leo kupitia uwanja huo, walichukuliwa na basi kupelekwa hotelini. Hivi ndivyo anavyoelezea:
Niliwasili Alfajiri ya saa kumi na moja nikitokea nchini South Africa nilikuwa napita kubadilisha ndege kurejea nyumbani Bongo Lakini maswahibu haya yaliyotokea majira ya saa 1 asubuhi huku mimi na abiria wengine tukisubiri kwenye ndege ghafla tulikuja kujuzwa kuwa hali ya usalama pale Airport haikuwa shwari na tulivyotoka kwenye ndege ndio niliposhudia uwanja wa ndege wa Kenya ukiwaka moto. Hadi sasa sasa chanzo cha moto ule uliosababisha kuwaka kwa Airport bado sijajua lakini hii imepelekea safari kukwama,sina uhakika kama tutaweza kuja Dar tena au Ndege kama zitaweza kuruka kwa leo maana hapa tulipo wanatupeleka hotelini. Imewalazimu uongozi wa Immigration kuja na kutugonga mihuri kwenye basi la wasafiri na kuwekewa usalama wa mabegi yetu.”
Hizi ni baadhi ya picha alizoweka kwenye blog ya Wasafi.
IMG-20130807-WA0001
IMG-20130807-WA0003
IMG-20130807-WA0004
IMG-20130807-WA0008
IMG-20130807-WA0010
IMG-20130807-WA0012
IMG-20130807-WA0013
IMG-20130807-WA0014
IMG-20130807-WA0015
IMG-20130807-WA0016
IMG-20130807-WA0017
IMG-20130807-WA0018
IMG-20130807-WA0019
IMG-20130807-WA0020
IMG-20130807-WA0021

No comments:

COMMENTS

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...