Akizungumza
jijini Dar es Salaam baada ya Stars kuwasili, Meneja wa Bia ya
Kilimanjaro Premium Lager, George Kavishe alisema licha ya habari hizi
kutokuwa njema kwa watanzania, ni vizuri kukubali matokeo na kuangalia
picha kubwa na malengo ya muda mrefu.
“Ni
vyema tukumbuke kuwa kwenye mpira kuna kushinda na kushindwa,” alisema
Bw Kavishe na kuongeza, “Tunapenda kuwahakikishia watanzania kuwa sisi
kama wadhamini hatujakata tama na bado tuna imani na timu hii na kocha
Kim Poulsen kwa hivyo tunawaomba watanzania wasife moyo.”
Alisema
wakati walipoanza kuidhamini Taifa Stars mwezi Mei mwaka jana na
kuwekeza zaidi ya shilingi bilioni mbili kwa mwaka, kwa muda wa miaka
mitano, walikuwa na malengo kadhaa ikiwemo kuinua hadhi ya Timu ya
Taifa, kuhakikisha wanaingia kambini kwa muda unaotakiwa, wanalipwa
vizuri, wanakula na kulala vizuri na kusafiri vizuri.
“Tumejitahidi
kufanya mambo haya kwani wachezaji sasa hivi wana DVD zenye maelezo
yao, tumewapa suti mpya na za kisasa na pia tumewapa basi jipya la
kisasa. Mambo haya yote pamoja na mambo wanayofundishwa na Mwalimu Kim
Poulsen yamesaidia kuleta mabadiliko kwa timu ya Taifa,” alisema.
Alisema
kuna mafanikio mazuri ya timu ya taifa ambayo watanzania lazima
wayakumbuke kama kuzifunga timu kama Zambia, Cameroon, Morocco na Kenya.
Kwa
mujibu wa Meneja huyo walipoanza udhamini Tanzania ilikuwa katika
nafasi ya 145 kwa mujibu wa FIFA lakini sasa imesogea hadi 109. “Haya ni
mafanikio makubwa kwani tumesogea hatua zaidi ya 40,” alisema.
Alisema
safari ya mafanikio katika mpira ni ndefu na inahitaji uvumilivu wa
hali ya juu na kuongeza kuwa Kocha Kim Poulsen anafanya kazi nzuri ya
kuibua vijana.
“Kocha
anahitaji kuungwa mkono na sisi sote kuanzia kwa TFF, sisi wadhamini na
watanzania wote. Tunahitaji kuangalia picha kubwa,” alisema na
kuongeza,”Nawaomba watanzania tuwe wazalendo wakati huu hii ni timu yetu
na tunatakiwa kujivunia. Vyombo vya habari pia viwe mstari wa mbele
kuonesha uzalendo.”
Alisema
mechi dhidi ya Gambia itakayochezwa mwezi wa 9 ya kuwania kufuzu Kombe
la Dunia ni muhimu hata kama Tanzania haisongi mbele kwani itasaidia
katika ngazi za FIFA.
source bin zubeiry
Wachezaji wa Taifa Stars wakiwasili jana usiku kutoka Uganda |
source bin zubeiry
No comments:
Post a Comment